Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya
asili mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa
kwa wiki tatu sasa.
Kutokana na maafikiano hayo kati ya serikali na
chama cha walimu nchini KNUT, sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu.
Hatua
hiyo sasa itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na
upili za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni.
Vyama
vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali kuwalipa
walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja.
Awali
serikali ya Kenya
ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali kulipwa
kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu.
Mwalimu
wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi 39.000.
Serikali
ya Kenya
imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa zaidi ya walimu 250,000 ambao
walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi.
Chanzo: BBC Swahili..
No comments:
Post a Comment