Friday, September 28, 2012

Zitto Kabwe asema hakuteleza kusema anagombe Urais mwaka 2015...


Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005. 

NB: Hii imetoka kwenye ukurasa wake wa facebook.... tembelea na wewe ujionee..

No comments:

Post a Comment