Thursday, September 27, 2012

Nigeria yaingia katika mzozo na Saud Arabia juu ya mambo Hija...


Nigeria imesitisha safari zake za ndege za Mahujaji wanaokwenda kuhiji Saudi Arabia baada ya nchi hiyo kuwarejesha zaidi ya wanawake mia moja na sabini waliowasili huko bila kufuatana na wanaume.
Spika wa Bunge nchini humo ataongoza Ujumbe kwenda Saudi Arabia kulalamika rasmi kwa jinsi Mahujaji wake walivyotendewa.
Mwanamke mmoja kati ya hao waliorejeshwa ameiambia BBC kuwa wakati wakiwa kizuizini hawakupewa chakula.
Hapo awali, bunge la Nigeria lilitoa wito kwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan kuwasiliana na mfalme wa Saudia, Abdullah kujaribu kumaliza mzozo uliozuka kati ya nchi hizo mbili kufuatia sakata ya Hajj.
Serikali ya Saudia iliwarejesha nyumbani zaidi ya wanawake miamoja na sabini ambao waliwasili nchini humo waliokwenda Hajj bila (Mahram) au mwanaume ambaye ni jamaa yake au mume wake
Wanawake wengine elfu moja wamezuiliwa hadi watakaporejeshwa nyumbani kwao.
Saudi Arabia imekuwa ikielezea wasiwasi kuhusu waafrika wanaokwenda nchini humo na kusalia huko baada ya kuhiji na hivyo kujiweka katika hali ya kuombaomba au hata kujiingiza katika biashara ya ukahaba.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment