Monday, October 1, 2012

Mnaotaka kuenda kuwaona watani wa jadi....


Release No. 159 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Oktoba 1, 2012 TIKETI YANGA, SIMBA KUANZA KUUZWA KESHO Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.

Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni. Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja. Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000.

Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000. Wakati huo huo, mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.

Boniface Wambura, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

 

No comments:

Post a Comment