Monday, October 1, 2012

Mzee Mwinyi na mkewe watoa msaada kwa wakazi wa kondoa..

 Mzee Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakiongozana na diwani wa kata ya Kwadelo Kondoa alipotembelewa nyumbani kwake na wakazi wa kijiji hicho kwa mwaliko maalum. Hapo ndipo alipoitaka Serikali kuwa sikivu kwa vijana.

 Alitoa msaada wa vitanda vya kujifungulia, mapipa ya maji na vitu vingine kwa wakaza wa kijiji cha Kwadelo kilichopo Kondoa.
Mama nae akisema chochote. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikilisikia jina la mama huyu likitajwa sana, lakini alipotea mara baada ya mumewe kumaliza muda wake wa urais. Hapendi kutajwatajwa na vyombo vya habari na wala harufu ya pesa hapendi mama huyu...


Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa matukio blogspot.

No comments:

Post a Comment