TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
leo zimetiliana saini Mkataba juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi
ambapo Zanzibar
itapatiwa jumla ya RMB 60 Millioni sawa na TZS,14.8 BILLIONI.
Kwa upande wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi Fedha ,Uchumi na Mipango ya Maendelro Omar
Yussuf Mzee ndie alietia saini na kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa
China Naibu Waziri wa Biashara Zhong Shan ndie alietiana saini ambapo
ulishuhudiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Idd na kwa
upande wa China Naibu Waziri Mkuu wa nchi Hui Liangyu.
Kwa mujibu wa Mkataba
huo wa Mashirikiano Zanzibar itafaidika katika Ujenzi wa Majengo mapya na
Ukarabati mkubwa wa Majengo yaliopo katika Hospitali ya Abdulla Mzee ..Pia
Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwananakwerekwe.Halkadhalika Zanzibar itafaidika
katika utiaji wa Taa za Barabarani zitakazotumia Nishati ya jua katika baadhi
ya Barabara kuu za Mjini.
Aidha Mkataba huo
unaelezea kuwa Zanzibar
itapata Mafunzo Mafupi na Marefu katika Fani tofauti ambayo itapendekezwa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Mbali na hayo pia kutakuwapo Uchimbaji wa
Visima vya Maji pamoja na maeneo mengine ambayo Nchi mbili zitakubaliana.
Pia ujumbe huo wa China
umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu
wanne(4) kutoka China ambao watakuwepo Zanzibar kwa miaka miwili(2) ambao
watawafundisha Mafundi wa Mitambo wa Studio yakurushia matangazo ya Redio
pamoja na kutoa Vifaa mbali mbali kwa ajili ya Studio hiyo.
Ujumbe huo wa China
ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu uliwasili Zanzibar leo jioni na kupokelewa na
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Viongozi mbali
mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwamo Mawaziri. Makatibu wakuu na
Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na maofisa mbali mbali wa Serikali.
Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein jioni hiyo hiyo
alikuwa na Mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu Ikulu ambapo
walizungumzia juu ya Ushirikiano kati ya Nchi zao.
Usiku huu Makamo wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Amemuandalia Chakula Naibu Waziri Mkuu
wa China
pamoja na ujumbe wake huko katika hoteli ya Lagemma Nungwi.
Kesho asubuhi Naibu
Waziri Mkuu wa China
na ujumbe wake watatembelea kanisa la Anglican Mkunazini na baadae kuelekea
Beit el Ajaib na Jumba la Wananachi Forodhani na kuelekea Uwanja wa ndege kwa
kurejea Dar es Slaam.
IMETOLEWA NA IDARA YA
HABARI MAELEZO ZANZIBAR
6/9/2012
No comments:
Post a Comment