Thursday, September 6, 2012

TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI



‘‘Mauaji Ya Waandishi Na Wananchi YatavurugaMchakato Wa KupataKatiba
Mpya Tanzania!’’

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumepokea taarifa za kuuawa kinyama
 
kwaMwandishi Daudi Mwangosi wa Channel 10na Mwenyekiti wa Chama cha
waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) kwa mshtukona masikitiko
makubwa. Kama ilivyokwishaelezwa na wengi, kifo cha mwandishi huyu ni
cha kwanza cha aina yake katika tasnia ya habari nchini na kinatishia
si tu uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa habari kwa ujumla wake, bali
pia kifo hiki na vingine vya siku za karibuni vinauweka mchakato wa
Katiba Mpya njia panda. Vitendo vya mauaji ya raia vinazidi kushamiri
siku hadi siku. Wapo wananchiwanaouawa na watu wanaoitwa wenye hasira
kali kwa tuhumaza uhalifu. Wapo raiawanaouliwa na majambazi na
wahalifu wenginekwa sababu ya ulinzi duni katika maeneowanayoishi.
Aidha, wapo pia wananchi wanaopoteza maisha yao kila siku kwa tuhuma
za kwamba ni wachawi.Ukiacha hao, idadi kubwa ya watanzania wanaishi
na ulemavu wa ngozi wamepotezamaisha kwa kukatwa viungo au kuuliwa
kabisa kwa imani za kishirikina. Hali sasa imefikia kuwa mbaya hadi
kuna watanzania wanajisikia salama zaidi wakiwa mwituni kuliko
majumbani. Yote haya yanasikitisha sanakwa ujumla wake! Haki ya kuishi
inayowekwa na kulindwa na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imeanzakuingia dosari katika Tanzania.Ukiacha mauaji
yanayofanywa na watu wasiojulikana au miongoni mwa raia, yamekuwepo
pia mauaji yanayozidi kuongezeka ya raia yanayofanywa na wawekezaji au
matajiri nchini. Zipo kesi kadhaa za mauaji ya namna hii.

Hayo nayo yamekuwa yakitokea kwa sababu ya ulinzi mdogo ambao wananchi
 
wanao kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Jeshi la Polisi,
ambalo ndio lenye dhamana ya kulinda watu na mali zaohaliwezi kukwepa
lawama katika aina zote hizo za mauaji. Itakumbukwa pia kuwa ajali za
magari, mabasi na meli zinagharimu sanamaisha ya watanzania katika
siku za karibuni. Kwa kiasi fulani, hata kukithiri kwa ajali hizi nako
kunahusishwa na mwenendo mbovu wa usimamizi wa vyombo vya usafiri
unaofanywa na idara mbalimbali za serikali ikiwemo kikosi cha usalama
barabarani. Roho zawatanzania zinazidi kupotea kutokana na udhaifu
mkubwa unaosababishwa na rushwa na mambo mengine ya ukosefu wa maadili
katika vyombo vya usimamizi wa haki. Mauaji ya raia yanayofanywa moja
kwa moja naaskari wa Jeshi la Polisi nayo yanazidi kuongezeka
sanakiasi cha kutishia amani na utulivu wa nchi yetu. Aidha, mauaji
yanayohusishwa na siasa nayo yanazidi kuongezeka na kuzidisha chuki ya
kisiasa ambayo ni mbaya sana kwa ustawi wa nchi yetu. Kwa mfano katika
miezi ya Karibuni, kumekuwepo matumizi ya nguvu kuzidi kiasi kwa raia
wanaokuwa wakipanga na kufanyamaandamano au mikusanyiko yenye lengo la
kujadili au kupinga jambo fulani. Matokeo yake, kumetokea majeruhi na
mauaji ambayo yamesababishwa na vurugu ambazo zinatokana na Jeshi la
Polisi kudhibiti vitendo halali vya wananchi. Kwasababu hiyo, JUKWAA
LA KATIBA TANZANIA tunatoa witoufuatao kwa Jeshi la Polisi na idara
nyingine za serikali zenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, malina
mipaka ya Nchi yetu:

1.1. Jeshila Polisi liache kutumia nguvu kuzidi kiasi katika matukio
 
yote ya kulinda mikutano na matukio ya hadhara. Tujuavyo sisi, Jeshi
la Polisi linalotumia risasi za moto, mabomu ya kivita, maji ya
kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya raia ambao hawajabeba hata
fimbo za kuchungia mifugo. Ni Jeshi lisilojiamini na linaloonesha woga
wa ajabu. Kwa hadhira kama za Nyololo, Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam
na nyinginezo miezi yaKaribuni, Jeshi la Polisi lingeweza kuwatuliza
wananchi kwa kutumia filimbi tu. Matumizi ya nguvu na kumwagia maji ya
kuwasha hata wazee wastaafu wanaodai haki zao inaweza kuwa ndio laana
inayopelekea Polisi kusikia furaha kuua kila mara. Ipo kanuni ya
kimataifa inayowataka Polisi kutumia nguvu kidogo sana inayolingana tu
na nguvu ya umma wanaokabiliana nao katika kutuliza ghasia.

2.Wakati huu wa mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania na
 
hata baada ya hapo, Jeshi la Polisi lijiepushe kuingilia shughuli za
Kisiasa kwa kuziunga mkono au kuzivuruga. Mikusanyiko mingi ambayo
imepelekea mauaji wakati polisi ikijaribu kuivunja ni matukio
yaliyolenga kupata majibu ya kisiasa na siyo ya kipolisi. Wajibu wa
Jeshi la Polisi

katika wakati kama huo ni kulinda na kuwezesha wananchi husika kueleza
 
madaiyao kwa uhuru na bila kuvurugwa na kundi jingine lolote la watu
wasiopendezwa na madai ya kundi husika. Tabia inayozidi kushamiri ya
Jeshi la Polisi kutaka kujibu au kuzima hoja za Kisiasa au kiuchumi
kwa mtutu wa bunduki, mabomu, maji ya kuwasha na virungu ni tabia ya
Jeshi kutaka kuingilia kazi isiyo yake na ndio maana inawashinda.
Aidha, kama Polisi wangekuwa niwataalam wa Siasa, wangegundua kuwa
wanachokifanya ni kuahirisha matatizo na si kuyatatua!

3. Jeshi la Polisi na vyombo venye dhamana ya ulinzi vijitambue upya
 
kuwa vina wajibu wa kulinda raia, mipaka na mali zao si vinginevyo.
Mauaji yanayoendelea nchini ni uporaji wa haki ya kuishi na haki
nyingine nyingi chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana
ile ya Zanzibar.Aidha, Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla wana
wajibu wa kuhakikisha na kudumisha ustawi wa wananchi kwa mujibu wa
ibara ya 8 (1) (b) nahawana mamlaka ya kuua raia. Ikumbukwe kuwa
mamlaka yote kikatiba katika Tanzaniayako kwa wananchi na serikali
pamoja na Jeshi lake la Polisi watapata madaraka na mamlaka hayo
kutoka kwa Wananchi. Nani amewapa Polisi mamlaka ya kuua watanzania?
Nani amewapa Jeshi la magereza mamlaka ya kuwapiga na kumwaga damu za
Waandishi? Nani amewapa askari wanyamapori mamlaka ya kupiga risasi
hovyo nakuua ng’ombe mbele ya wenye maliyao?

4.Athari za matukio ya mauaji na fujo zinazosababishwa na Jeshi la
 
Polisi kutawanya waandamanaji au mikusanyiko mingine ni kubwa sana
katika kuathiri vibaya hamasa ya wananchi kwenye Mchakato wa Katiba.
Mpaka sasa, tayari watu wengi wameingia wasiwasi na wameamua
kutoshiriki mikutano ya kutoa maoni ya Katiba inayoendeshwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba nchini. Endapo Jeshi la Polisi halitaacha kuua na
kutishiaraia kwa kila wanachokifanya, mchakato wa Katiba utavurugika
kabla Katiba mpya haijapatikana. Kwa mwenendo wa sasa, Jeshi la Polisi
litakuja kupiga mabomu na kuua hata wananchi watakapokuwa katika
Mabaraza ya Katiba wakijadili na kupinga baadhi ya vipengele
vitakavyoingizwa katika rasimu ya Katiba. Pia, itafika wakati wananchi
watataka kuandamana kwa amani kuunga mkono au kupinga mambo Fulani
katikaKatiba. Kwa hali ilivyo, Jeshi la Polisi litaona hiyo ni fursa
ya kutumia mabomu na risasi kuzuia wasiseme wanayotaka kusema. Hii ni
hatari kubwa sana!

5. Mikusanyiko, maandamano na shughuli za mikutano ya Siasa ni matendo
 
halali na haki ya kila mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano, 1977 ibara ya 8, 20 na 21. Suala la kutoa taarifa kwaJeshi
la Polisi kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi ni suala la
kuwajulisha tu kwa lengo la kuwaweka tayari endapo kutahitajika msaada
wa Jeshi la Polisi wakati wa shughuli kamahiyo. Tabia iliyoota mizizi
ya Polisi kujiona kama wamepewa taarifaili watoe au kukataa kibali ni
uelewa finyu wa Katiba na sheria za Nchi. Ipo haja ya kuongeza uelewa
wa wasimamizi wetu wa sheria ili wawe na uelewa mpana wa sheria na
ibaraza Katiba wanazozisimamia badala ya kujiona kama wana wajibu wa
Msajili wa vyama vya Siasa wa kuratibu shughuli za vyama. Mikutano,
mikusanyiko, mihadhara, maandamano na mijadala ni haki ya Kikatiba ya
Kila mtanzania binafsi na kwa makundi. Kwa kuwa haki ya kuishi
iliyoporwa kwa MwandishiDaudi Mwangosi ndio haki kubwa kuliko zote,
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunataka jambo hili lisiishiekuunda Tume za
uchunguzi pasipo kufanyia kazi mapendekezo yake. Aidha, kwa kuwa
uchunguzi unaofanywa hauhusiani na kilichomuua ndugu Mwangosi wala
kundi gani limemuua, tunapendekeza busara itumike kwa viongozi wa
Jeshi la Polisi, kuanzia Kamanda wa Polisi Mkoawa Iringa kuachia ngazi
ili kupisha uchunguzi huru wa Tume itakayoundwa na Mheshimiwa Rais
ikihusisha na kuongozwa na mhimili wa Mahakama. Taarifa ya uchunguzi
ipelekwe Bungeni na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kujadiliwa na ushauri
wa kibunge. Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
tunaitamka rasmi kuwa batili kwa kutumia kanuni ya sheria za kiasili
inayosema kuwa mtu au kundi hawezi kuwahakimu wa kesi inayomhusu
mwenyewe. Bila kufanya hivyo, tunapata wasiwasi kama Tume ya namna
hiyoinaweza kufanya kazi yake kwa uhuru. Kuachia ngazi kwa Kamanda wa
Polisi mkoani Iringa kutakuwa ishara kuwa Jeshi la Polisi linahitaji
kuwa makini zaidi katika kufanya kazi yake ya kulinda amani, mali na
maisha ya watanzania. Kwa sasa, zipo hisia kuwa Jeshi la Polisi lipo
juu ya sheria na Katiba, jamboambalo tunapenda kulikanusha vikali!

Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa serikalikutangaza rasmi kuwa itachukua
 
jukumu la kutunza, kusomesha, kulisha na kuhudumia familia aliyoiacha
Daudi Mwangosi kuanzia sasa kwa muda wa miaka 20 watakapoweza
kujitegemea wenyewe. Itakuwa ni fedheha kuiona familia aliyoianzisha
Marehemu Mwangosi ikisambaratika kwa sababu kichwa cha nyumba hiyo
kimesambaratishwa na bomu la Polisi ambalo kodi yake
Mwangosiilichangia kulinunua. Kufikia hapa, tunapenda kutangaza rasmi
kuwa msiba huu nimsiba wa KIKATIBA na tunaomba ufahamike hivyo kwa
umma wote wa watanzania na kote duniani.

Mungu ailazeroho ya Marehemu Mwanahabari Daudi Mwangosi mahali pema
 
peponi Amina!

Imetolewana kusainiwa kwa niaba ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA,
 
Deus MKibamba
Mwenyekiti
Alhamis, 06 Septemba 2012

No comments:

Post a Comment