Hapa Waziri Nchimbi aliwataka watu wote kusimama dakika moja kuomboleza kifo cha Mwandishi Daud.
Waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi akijinasibu kuwa yeye ni muumini wa haki hapendi dhulma.
Maafisa wa jeshi la Polisi wakimsikiliza kwa makini bosi wao Waziri Dk Emmanuel Nchimbi.
NA Hafidh Kido
Waziri wa mambo ya ndani
Dk Emmanuel Nchimbi ameshangazwa na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini
IGP Said Mwema juu ya mauaji ya mwandishi yaliyotokea Mkoani Iringa wiki
iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi la
polisi nchini wakati akitaja majina matano ya watu watakaokuwa katika tume
aliyoiunda kuchunguza mauaji hayo.
Dk Nchimbi alisema haamini kama IGP Mwema anastahiki nafasi hiyo
maana amekuwa mpole sana
kabla na baada ya tukio la Iringa mbali ya kupokea ujumbe wa simu kutoka kwa Dk
Slaa uliomtaka kuandaa silaha za kutosha kukabiliana na mauaji yatakayotokea.
“Mimi nilishangaa sana
namna IGP alivyomnyenyekea katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilbord Slaa tarehe 28
mwezi uliopita juu ya kusitisha maandamano na mikutano ya chama hicho ili
kupisha sensa. Maana alimnyenyekea na kumbembeleza utadhani anamuomba nini
sijui, mpaka nikajiuliza huyu ni IGP kweli.
“Kama hiyo haitoshi tarehe moja
mwezi huu siku moja kabla ya mauaji ya Iringa IGP alipokea ujumbe wa simu
kutoka kwa DK Slaa kumtaka kuandaa silaha za kutosha kukabiliana na karamu ya
mauaji siku ya pili. Lakini alipuuza na kweli mauaji yalitokea,” alisema
Nchimbi.
Ujumbe huo wa simu uliotumwa kwa IGP Mwema kutoka kwa DK Slaa
ulisomeka hivi “IGP nasubiri simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za
kutosha, mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea,
mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hegue. Ni afadhali kufa kuliko manyanyaso
haya.”
Mbali na hayo Dk Nchimbi aliwaasa wanahabari kutoshabikia mambo
haya yanayoendelea nchini na kuhoji ikiwa chadema wanafurahia mambo yanayotokea
ama nao wanahuzunika.
“Hebu tujiulize kwa pamoja ndugu zangu, hawa chadema hawajui
umuhimu wa sensa ama wanafanya kusudi. Na walishawahi kujiuliza ndani ya miezi
mitatu mikutano yao
mitatu imeua watu watatu familia za marehemu hawa zinakuwa katika hali gani.
Mbona wapo wanaharakati kabla yao
walifanya harakati bila mauaji,” alihoji Dk Nchimbi.
Aidha katika mkutano huo Waziri Dk Nchimbi alitaja majina ya
wajumbe watano watakaokuwa katika tume huru ya kuchunguza mauaji hayo na kuwapa
siku thalathini kumletea majibu ya kueleweka.
“Nimeunda tume ya watu watano itakayokuwa chini ya uenyekiti wa
jaji mstaafu Time Ihemba, nikawaambia jukwaa lawahariri wanipe jina moja
wakanipa jina la Teoful Makunga, pia nikawaomba MCT wanipe jina moja wakanipa
Pili Mtambalike. Wakati jeshi la wananchi Tanzania wamenipa mtaalamu wa
milipuko kanali Wema W.Wapo, na upande wa jeshi la polisi tunae kamishna Esaya
Mkulu.
Tume hii itakuwa huru na ya haki hakuna kupendelewa wala kushindwa
kwa jambo lolote lile, na nimeshawaambia ikiwa watakuwa na tatizo lolote la
kitaalamu wasisite kuwasiliana na wizara ili tuombe msaada kutoka nje” Dk
nchimbi.
Akifafanua masuala ya msingi ambayo yataangaziwa katika tume hiyo
Dk Nchimbi alisema, yapo mambo sita ambayo mpaka sasa ndiyo yanayotajwatajwa na
watu katika mitandao ya kijamii na hata jukwaa la wahariri walitaja baadhi.
“Yapo mambo sita ambayo yatakuwa kama muongozo kwa kamati hii, Kwanza nini chanzo cha mauaji, bomu, risasi ama nini.
Pili ni kweli upo uhasama baina ya jeshi la polisi na waandishi wa mkoa wa
Iringa. Tatu, ni kweli wapo waandishi watatu ambao inadaiwa jeshi la polisi
mkoani humo wamewaweka katika orosha ya kuwashughulikia.
“Nne, ukubwa wa nguvu iliyotumika kumkamata Marehemu Daud Mwangosi
na wafuasi wa chadema ilikuwa na uhalali wowote. Tano, Vyama vya siasa ni kweli
wamepanga kukata rufaa mara wasiporisdhishwa na tume ya polisi iliyoundwa
kuchunguza tukio hilo .
Na mwisho ni kutaka kujua kuwa ni kweli mkoani Iringa upo mvutano wa muda mrefu
baina ya jeshi la polisi na vyama vya siasa,” alieleza Dk Nchimbi.
Katika hatua nyingine jembe lenu lilimuuliza Waziri Dk Nchimbi
ikiwa atakuwa tayari kuwajibika mara baada ya ripoti ya tume hiyo kutolewa na
kubainika jeshi la polisi lilihusika moja kwa moja na mauaji hayo.
Majibu yake yalikuwa haya “Mbona unaharakisha majibu ya tume namna
hiyo, labda niwaambie kitu mimi ni muumini wa haki na ikiwa itabainika kuna
kuchezewachezewa haki kila aliehusika atawajibishwa kwa mujibu wa sheria.”
Lakini baada ya jembe kusisitiza kutoridhishwa na majibu yake
kwani swali la msingi lilikuwa ni yeye akiwa waziri ambae jeshi la polisi lipo
chini yake atakubali kuwajibika.
Alijibu kwa hamaki “mbona hamunielewi na mnasisitiza vitu kama hivyo, mimi jamani nikiondoka mtanikumbuka shenziii,”
alihamaki Dk Nchimbi.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
04/09/2012
No comments:
Post a Comment