Sunday, September 2, 2012
Niliogopa kuweka habari hii kabla sijaithibitisha. Ingawa niliipata mapema....
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa Daud Mwangosi, ambae pia ni mwandishi wa kituo cha Channel Ten kutoka Iringa ameuwawa kwa bomu wakati wa vurugu zilizotokea mkoani Iringa ambapo wafuasi wa cahma cha siasa CHADEMA walipobishana na jeshi la polisi.
Taarifa ambayo sijaithibitisha ni kuwa bomu hilo lilitupwa na polisi ama wafuasi wa CHADEMA, maana mwandishi ambae amenithibitishia habari hizi aliekuwa eneo la tukio amepelekwa huko na msafara wa DR Slaa ambae ni katibu mkuu wa CHADEMA, yeye ameniambia bomu hilo lilirushwa na polisi. inawezekana amesema hivyo kwakuwa amepelekwa huko na CHADEMA.
Lakini ukweli utabainika leo usiku wakati wa taarifa ya habari tusubiri. Ila hali ni mbaya kama tumefikia hapa, mpaka askari wanadriki kuwatupia bomu raia hakika hali ni mbaya. Kumbuka wiki iliyopita mkoani Morogoro askari waliua muuza magazeti wakati wa vurugu za CHADEMA....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment