Tuesday, September 4, 2012

Saa za Mwisho za Jembe Daud Mwangosi...

 Hapa akishushwa katika nyumba yake ya milele Kijijini kwa Busoka, kata ya Utete Wilayani Rungwe Mkoa wa  Mbeya leo.
                                     Mke wa marehemu akiangalia sura ya mwisho ya Mumewe Kipenzi.

 Waziri asie na wizara maalum Prof Mark Mwandosya na Mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la Jembe Daud.

Dk Slaa, Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, akiweka shada la maua.

Jembe Daud Mwangozi alifariki kwa bomu wakati wa vurugu za polisi na cahdema mkoani Iringa wakati akijaribu kumtoa mikononi mwa polisi mwandishi wa nipashe aliekamatwa katika vurugu hizo. Lakini Jeshi la polisi lilimpiga na kumlipua na bomu mpaka kusababisha mauti yake.

Wazri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi leo ameunda tume ya watu watano itakayochunguza tukio hilo. Jembe Mwangosi ameacha mjane na  watoto wanne.

Picha zote kwa hisani ya  
http://mbeyayetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment