Sipendi kukengeuka taaluma, kawaida picha za kutisha kama hizi hazifai kuwekwa kwenye mitandao ama magazeti. Lakini nimeamua kufanya kinyume ili wanaadamu kote duniani waone kilichofanyika huko Iringa kwa mwandishi mwenzetu.
Huu ndiwo mwili wa Marehem Daud, mwenyekiti wa chama cha wanahabari Iringa na mwandishi wa kituo cha channel ten Iringa.Inadaiwa amepigwa bomu na jeshi la polisi, ingawa wao wanapinga.
Lakini leo wakati nikisikia taarifa ya habari, mkuu wa jeshi hilo mkoani Iringa amekataa na kusema kuna kitu kilirushwa kutoka kwa wananchi na ndicho kilichomuua. Sasa ikiwa wananchi wananweza kumiliki silaha kali kama mabom ya kurusha kwa mkono; jeshi letu linatuambia nini kuhusu usalama wa raia?
Na leo wamesema kuwa wametuma kikosi kuenda kuchunguza tukio hili, kweli haki itatendeka? maana mpaka Ndugu yetu roho inaacha mwili kwa utumbo kutoka nje alikuwa mikononi mwa polisi tena akipokea kipigo kikali, je uchunguzi utatoa matokeo ya kweli? Tusubiri....
No comments:
Post a Comment