Friday, September 7, 2012

Waislamu waandamana Dar kushinikiza wenzao waachiwe...

 mkuu wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiwaasa waisla, kuwacha jazba wamsikilize kwani alikuwa anatoa taarifa njema za kuwaachia wenzao...

Waislamu wakiwa wamekaa katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa saa zaidi ya tano ambapo walipomaliza sala ya ijumaa tu walifanya maandamano kutoka misikiti yote ya mjini mpaka zilipo ofisi za wizara hiyo. Walikaa mpaka sala ya alasiri ilipowakuta wakatayamam kwa kutumia vumbi na kusali.

Baada ya hapo viongozi wa juu wa jeshi hilo pamoja na maafisa wa wizara wakiongozwa na waziri Dk Emmanuel Nchimbi, ambapo walikubaliana kuwaachia watu hao waliokuwa na kesi ya kukataa kuhesabiwa katika sensa ya mwaka huu. Lakini taarifa zinasema waislamu hao hawajaachiwa moja kwa moja bali wapo nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment