Tatizo la kukosa
usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kusahau au
''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana
maumbile yanayofananishwa na binadamu.
Vipande vya protini, kwa lugha
ya kitaalamu (plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti
inayosababisha maradhi haya.
Utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika
jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za
uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo
kwa viumbe hao.
Taasisi
inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK ) imehimiza
kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa
Madaktari.
Utafiti
wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelekea
kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo.
Wagonjwa
hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa
maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika
kiasi kwamba tiba inakua vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo
sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama
mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza.
Viwango
vya protini ijulikanayo kama Beta Amyloid
kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi
cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga uchafu usiofutika kwenye
ubongo na maradhi ya Alzheimer.
Majaribio
yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington
yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa
kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza
kusinzia kwa dakika 30 pekee.
Mmojapo
wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika
usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo
yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
"ikiwa
matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua
kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu
tofauti kabisa."
Hata
hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa
binadamu kwa sababu nyingi zinazosababisha kutatizika na usingizi.
Dr
Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's Research UK , ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima
binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya
matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.
Aliongezea
kuwa: "tayari umekuwepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi
huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha
kuwa kuna uwezekano wa kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara
na onyo la maradhi ya kusahau au Alzheimer.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment