Sunday, September 2, 2012

Zenawi azikwa leo na maelfu kutoka bara lote la Afrika..Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akijiandaa kuweka shada la maua katika kaburi la Zenawi leo.


Sifa na salamu zinatolewa juu ya waziri mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia aliyeongoza kwa miaka mingi, ambaye anazikwa katika mji mkuu, Addis Ababa.
Maelfu ya wananchi wa Ethiopia - wengi wao wakiwa wamevaa T-shirt nyeusi zenye picha ya Bwana Meles - wamejaa kwenye medani kuu ya Addis Ababa.Viongozi wa Afrka na kwengineko wamekuwa wakionesha heshima zao pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alisema Bwana Meles alitumia upeo wake mkubwa kuendeleza Afrika.
Bwana Meles anasifiwa kuwa aliongoza maendeleo ya Ethiopia, lakini piya alilaumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu.
Aliyechukua nafasi yake, Hailemaruiam Desalegn, ataongoza nchi hadi uchaguzi wa mwaka wa 2015.
Chanzo: BBC Swahili..

No comments:

Post a Comment