Sunday, September 2, 2012

Mali hakukaliki...


Wakuu wa Algeria wanasema wanachunguza ripoti kuwa mwanabalozi mmoja wa Algeria ameuliwa na wapiganaji wa Kiislamu wa siasa kali nchini Mali.

Vuguvugu la Umoja na Jihadi Afrika Magharibi, ambalo linadhibiti karibu eneo lote la kaskazini mwa Mali, limetoa taarifa kwenye mtandao wa internet likisema kuwa limemuuwa mwanabalozi Tahar Touati.
Wanabalozi saba wa Algeria walitekwa nyara mwezi wa Aprili kutoka ofisi yao ya balozi mdogo kaskazini mwa Mali.
Kundi hilo limeitaka serikali ya Algeria iwaachilie huru wapiganaji wa Kiislamu waliotekwa karibuni kusini mwa nchi, pamoja na kiongozi wa tawi la Al Qaeda kaskazini mwa Afrika.
 Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment