Habari zenu ndugu zangu, poleni kwa kuwatupa sikukuu imetufanya kuenda mbio. Sasa imeisha turudi ofisini. picha hii na habari yake nilivipata katika ukurasa wa facebook wa ndugu Chesi Mpilipili. Nimevutiwa sana na hii habari nikaona si vibaya tukigawana taarifa.
...Huyu alikuwa ni Nguli wa muziki ambaye
tunaweza kusema ni kama 'alinunua' kifo chake
mwenyewe kwa maana halisi.
Alizaliwa Washington D.C tar 2 April 1939 kwa baba Marvin GAY Sr aliyekuwa
mchungaji na mama Alberta Cooper-GAY aliyekuwa mwalimu na mtumishi wa ndani.
Alibatizwa Marvin Pentz GAY na kama ilivyo kwa
wasanii wengi wa zamani wa Marekani alianza kwa kuimba kwaya kwenye kanisa
alilokuwa akihubiri baba yake.
Alipoanza rasmi safari ya kuwa mwanamuziki akaongeza herufi e kwenye jina lake
la mwisho na kuanza kufahamika rasmi kama
MARVIN GAYE Jr.
Alipata kujifanya kichaa ili kutimuliwa
kwenye jeshi la anga la marekani USAF ili kutimuliwa baada ya kuwa mkaidi wa
kufuata amri za jeshi. Akarudi uraiani na kuingia rasmi kwenye shughuli za
Muziki.
Alisumbua sana na nyimbo zake za mapenzi kama 'How sweet it is(to be loved by
you), Aint no Mountain high enough, Heard it over the Grapevine, Aint that
peculiar, what is going' nk.
Hata hivyo, kilele cha mafanikio ilikuwa pale September 1982 alipotoa wimbo
uliokuja kuwa 'Wimbo wa Taifa wa Masuala ya Mapenzi' wa SEXUAL HEALINGS'
uliotingisha Ulimwengu mzima.
Matumizi ya madawa ya kulevya yakamfanya nguli huyu mtu asiyejiamini na kila
saa kuhisi kuwa kuna wabaya walikuwa wanamvizia ili kumdhuru na kwenye sikukuu
ya Krisimasi ya 1983 akamnunulia baba yake mzee Marvin Gay bastola ili aitumie
katika kumlinda. Ole Wake!
Miezi mitatu tu baadaye kwenye siku ya Wajinga tar 1 April 1984 baba mtu huyu
ambaye tayari aliishakuwa mtu wa kibywaji kwa sana akatumia bastola hiyo hiyo
kumuua mwanaye Marvin Gaye ambaye alikuwa anajaribu kusuluhisha mzozo kati ya
Wazazi wake hao.
MARVIN GAYE akatangulia mbele za haki siku moja kabla hajatimiza miaka 45
kamili huku kibao chake cha SEXUAL HEALINGS kikiwa kwenye kilele cha mafanikio
kama ilivyo hadi leo unapokisikia. MARVIN GAYE, tunakukumbuka:
No comments:
Post a Comment