Monday, August 27, 2012

Taarifa zaidi juu ya Kifo Cha Sheikh Aboud Rogo.

Maiti ya Sheikh Aboud Mohammed Rogo ikiwa katika gari baada ya kupigwa risasi leo mchana mjini Mombasa nchini Kenya.

Hii ni picha ikionyesha hali ya vurugu mjini Mombasa ambapo inaarifiwa kuwa Waislam mjini mombasa wamechoma kanisa moja na kujaribu kuchoma jingine bila ya mafanikio. lengo likiwa ni kuonyesha hasira zao baada ya kuuwawa Sheikh wao.





Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiislam nchini Somalia la al-Shabab.

Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makuruta wapya.


Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.

Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye orodha ya Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Julai, mwaka huu kwa kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.

Aidha mwezi huo huo wa Julai mwaka huu Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo vya usafiri na pia kuzuia mali zake 
wakisema alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa vifaa vya kisasa.

Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.

Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Sheikh huyo inasadikiwa amekuwa akiisumbua Serikali ya Kenya tangu mwaka 1998 kwa kesi za kigaidi kila kukicha lakini amekuwa akiishinda Serikali hiyo huku akizidi kujijengea umaarufu katika jamii za kiislamu nchini humo.

Inasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita katika mtaa wa Bamburi mjini humo.,

Aidha Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo amezikwa baadaye saa za mchana hapohapo mjini Mombasa.

Baada ya taarifa za kuuwawa kwa bwana Rogo, vijana wenye hasira walisambaa katika mitaa ya mji wa Mombasa wakiishutumu Serikali ya Kenya kwa uonevu dhini ya viongozi wa dini ya Kiislamu.

Vurugu hizo mpaka sasa zimesababisha gari ya polisi na Kanisa moja kuchomwa moto pamoja na kifo cha mtu mmoja.

Kidojembe itaendelea kukupa taarifa zaidi..........



No comments:

Post a Comment