Tuesday, August 21, 2012

Jembe Hasanoo afanya mambo Mkoa wa pwani..

Chama cha soka mkoa wa pwani (COREFA), kimeanza mazungumzo na mashirika ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuweza kujenga uwanja wa kisasa wa michezo katika mkoa huo baada kupata eneo walilokuwa wakilitafuta kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa COREFA Hassan Hasanoo, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa eneo hilo ambalo lipo mlandizi, Pwani linatosha kujenga uwanja huo wa kisasa utakaojumuisha michezo mbalimbali.
Hasanoo alisema kuwa uwanja huo utakapokamilika utachochea maendeleo ya mchezo wa soka katika mkoa huo, hasa katika kipindi hiki ambacho wanajipanga kuongeza timu zitakazocheza ligi kuu badala ya mbili zilizopo ambazo ni Ruvu Shooting na JKT Ruvu. Lengo ni kuhakikisha vijana wa mkoa huo wanahamasika katika michezo na wakati huo huo kunufaika kibiashara mara uwanja huo utakapokamilika.
Alibainisha kuwa tayari chama chake kimeanza mazungumzo na baadhi ya mashirika ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya kuingia nayo mikataba ya ujenzi huo. Na kudai mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na badala ya kukamilika ujenzi wa uwaanja huo utaanza mara moja na COREFA imepanga ukamilike miaka miwili ijayo. 
Itakumbukwa kuwa Hassan Hasanoo ni kiongozi wa chama cha soka pekee ambae hapendi kuonekana katika vyombo vya habari bali hufanya kazi ambazo huonekana matokeo yake baada ya kukamilika, na asilimia kubwa ya miradi anayoitimiza katika mkoa wa pwani pesa anatoa mfukoni mwake ama kufuata wafadhili ambao husaidia kusukuma gurudumu la michezo mkoani humo. <

No comments:

Post a Comment