Thursday, August 30, 2012

Hii imekaaje?

Kwa wasiomjua Hamad Rashid Mohammed, ni miongoni mwa waasisi wa chama cha siasa cha CUF, miezi michache walikuwa na malumbano katia chama hicho na kufikia kufukuzwa na katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad.

Lakini mbunge huyi wa Wawi Zanzibar, alipinga uamuzi huo wa kufukuzwa katika chama na kufungua kesi mahakama kuu ambayo iliweka pingamizi kufukuzwa kwake. Ila kesi bado inasikilizwa. Katika hatua nyingine inadaiwa Hamad Rashi ndie alieanzisha chama kipya cha ADC ambacho juzi kilipata usajili wa kudumu.

Ila yeye alipinga kuanzisha chama hicho ila cha ajabu juzi katika mkutano wa ADC alitokelezea na kushangiliwa sana..

No comments:

Post a Comment