Monday, August 27, 2012

Mombasa hakukaliki


Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa kiisilamu Aboud Rogo, ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la Al shabaab nchini Somalia kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa nchini Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa
Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.

Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Huyu ndie Sheikh Aboud Rogo enzi za uhai wake..

 Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment