Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki
akiwa angali madarakani.
Tangu
mwaka 2008, hili limefanyika mara kumi na tatu kote duniani -lakini kumi kati
ya viongozi hao wamekuwa marais wa nchi za afrika.
Kwa
nini vifo kama hivi vinatokea sana
barani Afrika?
Makundi
makubwa ya watu walikusanyika kushuhudia jeneza la hayati waziri mkuu wa Ethiopia meles Zenawi
lilipokuwa likipitishwa katikati mwa mji mkuuAddis Ababa , mnamo siku ya Jumanne wiki
iliyopita. Alifariki akiwa na umri wa miaka 57, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
lilipokuwa likipitishwa katikati mwa mji mkuu
Mapema mwezi huu, maelfu ya wananchi wa Ghana
walihudhuria mazishi ya hayati rais, John Atta Mills, aliyefariki ghafla akiwa
na umri wa miaka 68.
Miezi
minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini Malawi
kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais Bingu wa Mutharika,
aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na mshtuko wa moyo.
Na
mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea
Bissau , Malam Bacai Sanha, alifariki katika
hospitali ya kijeshi mjini paris
baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.
Kwa
hivyo viongozi wanne wa Afrika wamefariki mwaka huu pekee . Bila shaka ni pigo
kwa nchi husika na huzuni kubwa kwa familia za viongozi hao. Lakini je
mwandishi wa habari atafsiri vipi matukio haya?
Swali hili bila shaka linasababisha tathmini
ya maisha ya viongozi hao.
"
Ukitafakari kidogo orodha ya viongozi wa Afrika waliofariki bila shaka ni
ndefu'' anasemaAllison. Tangu mwaka 2008, viongozi 10 wa Afrika wamefariki
wakiwa madarakani.
Viongozi
wengine wa Afrika waliofariki wakiwa madarakani ni pamoja na Muammar Gaddafi
akiwa na miaka 69. Aliauawa wakati wa mapinduzi ya kiraia nchini Libya Oktoba
mwaka 2011
Aliyekuwa
rais wa Nigeria
Umaru Yar'Adua aliaga akiwa na miaka 58 mwezi Mei mwaka 2010 kutokana na
maradhi ya figo pamoja na moyo.
Omar
Bongo wa Gabon
akiwa na miaka 73 alifariki mwaka 2009
Raia
wa Guinea Bissau president, J B Vieira umri wa miaka 69 aliuawa mwezi Machi
mwaka 2009
Rais
wa Guinea Lansana Conte aliaga akiwa na miaka 74 mwaka 2008, kutokana na sababu
zisizojulikana.
Aliyekuwa
rais wa Zambia
, Levy Mwanawasa akiwa na miaka 59 mwaka 2008, kutokana na kiharusi.
Bila
shaka ni kweli kuwa viongozi wengi wa Afrika wanaaga dunia wakiwa wangali
madarakani kuliko katika bara lengine lolote duniani. Katika kipindi hicho ni
viongozi watatu pekee waliofariki wakiwa wangali madarakani kwingineko duniani.
Kim
Jong Il wa Korea kaskazini ,
rais wa Poland , Lech
Kaczynski, aliyefariki katika ajali ya ndege na David Thomson wa Barbados ,
aliyefariki kutokana na saratani.
Jibu
la wazi ni kuwa marais wa Afrioka ndio wakongwe zaidi kuliko marais wa mabara
mengine.Tathmini inayotolewa hapa ni kuwa waafrika wanapenda wenyewe kuwa na
viongozi wazee kwani kulingana na utamaduni , wanapata heshima kubwa kutoka kwa
jamii.
Muda
mrefu zaidi ambao marais wa Afrika wanaweza kuishi inakadariwa kuwa miaka 61
sawa na bara Asia . Viongozi wa bara la Afrika,
umri wao unakakadiriwa kuwa miaka 55 wakati barani Afrika rais mkongwe zaidi
anakadiriwa kuwa na miaka 59.
Lakini
kitu kingine cha kutafakari ni umri mrefu zaidi wanaoishi watu wa bara hilo ikikadiriwa kuwa chini sana
barani Afrika ikilinganishwa na mabara mengine kama Uropa, Amerika ya kusini na
barani Asia .
Sababu
kuu hapa ikiwa ni janga la ukimwi, na pia miundo msingi duni ya afya ambayo
inachangia idadi kubwa ya vifo hasa miongoni mwa watoto wachanga.
Lakini
umaskini katika maisha ya ujana na kwa watoto wachanga pia zinaathiri kubwa
katika umri wa mtu kulingana na daktari George Leeson wa chuo kikuu cha Oxford .
"marais
wa Afrika kabla ya kuchaguliwa huenda waliishi maisha ambayo sio mazuri sana na bila shaka hilo
litaathiri maisha yao
uzeeni'' anasema daktari Leeson.
Kwa
hivyo wakati wanapoingia madarakani, licha ya kuwa sasa wanaishi maisha ya
kifahari zaidi kuliko siku zao za utotoni, bado athari za maisha duni
walipokuwa wachanga huwaandama
Lakini
hii haimaanishi kuwa viongozi wote wa Afrika waliishi maisha duni walipokuwa
wadogo. Kuna mambo mengine chungu nzima ya kuzingatia. Mfano, siasa, dhana
kwamba, viongozi wa afrika wanapenda kung'ang'ania madarakani, hadi
watapofariki. Lakini dhana hii ingali kuthibitishwa.
Lakini
kunao viongozi waliong'ang'ania madaraka hadi wakafa, kama
vile Omar Bongo, Conte na Gaddafi, kulingana na tathmini mbali mbali. Lakini
wengine kama Meles Zenawi waligandia tu madarakani , kwa sababu kama Zenawi, alikuwa na miaka 57 pakee.
Hata
hivyo ni muhimu kujua kuwa tathmini hii ni ya viongoiz tu waliofariki wakiwa
ofisini tangu mwaka 2008.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment