Hapa Jembe nikitoka nyumbani kuelekea Msikitini..
Leo asubuhi nilialikwa na Dada Iptsam.... Hapa Dada Arafa akituandalia mazingira ya kula mapochopocho.
Kariakoo hii asubuhi, tazameni viungo vya pilau vilivyopata soko siku ya leo. Havikamatiki kabisaa..
Huyu wa katikati anaitwa Issa Shomari, sijaonana nae miaka yapata mitano. Nimeonana nae leo Kariakoo, Issa nilisoma nae sekondari Masjid Qubah Seminari. Ndie mwanafunzi pekee darasani kwetu aliefaulu na kupelekwa kidato cha tano shule ya serikali Lindi..
Kuku wa pilau huyu..
Huyu ni Sam Maela wa ITV akirekodi watu wanaosherehekea sikukuu mitaani.
Wanafunzi hawa wakiimba sikukuu mitaa ya kariakoo...
Abbas huyu akienda msikitini kizungu..
Waumini wa kiisalmu katika harakati za kusali Eid...
Jamani kama nilivyowaambia nimealikwa leo. Na waswahili husema uji wa matanga hauunganishi udugu. Maana nami nimealikwa hivyo siwezi kumualika mtu, poleni marafiki.
Mtoto wa dada Iptsam nae anashangilia sikukuu, anaitwa Manal huyu jamani.....
No comments:
Post a Comment