Na Mahmoud Zubeiry
BEKI mpya wa Yanga,
Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na
mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari kuelekea makao
makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam .
Hakuna kiongozi yeyote
wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa kuna tishio
kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda , mwenye asili ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli dola za
Kimarekani 30,000.
Inadaiwa, kabla ya
kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua
dola 30,000.
Hata hivyo, baadaye
mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba
kupitia viongozi wa APR na St
Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.
Lakini viongozi wa
Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika
hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo,
ili Simba wakazichukulie hapo.
Twite aliianza
kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali ,
Rwanda kwa
ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile
kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar
es Salaam,
Lakini upande wa pili,
Simba SC
waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa
kumtegea akitua nchini wamkamate.
Ametua na amekwenda
Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.
No comments:
Post a Comment