Wednesday, August 29, 2012

Leo mkutano wa wabunge wa Afrika Mashariki watokao Tanzania wameshindwa kufanya mkutano wao baada ya umeme kukatika idara ya habari Maelezo. Hivyo umeahirishwa mpaka jumapili asubuhi. Si aibu hii...?

 Hapa naibu mkurugenzi wa MAELEZO akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya kushindwa kufanyika mkutano huo kutokana na kukatika umeme katika jenmgo hilo la serikali ambalo halina hata jenereta.

 Wabunge hawa wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka kushoto Adam Kimbisa, Makongoro Nyerere, huyu simjui na anaefuata ni Shy Rose Banj. Hata sijui wanafurahia nini wakati mkutano wao umeshindwa kufanyika kutokana na hitilafu za umeme na wao ni wabunge wanachekelea tu....

Hapa wakijadiliana kabla ya kuondoka ukumbi wa idara nyeti ya habari MAELEZO... Mpaka jumapili asubuhi, nani aje!!!/.

No comments:

Post a Comment