Rais wa Afrika Kusini,
Jacob Zuma, amesema kuwa ataunda tume ya uchunguzi baada ya polisi kuwafyatulia
risasi maelfu ya wafanyikazi wa migodi waliogoma siku ya Alhamisi.
Polisi wanasema watu thelathini na wanne (34) waliuwawa katika tukio hilo .
Rais
wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association
of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka tume huru ya
kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa
ghasia hizo.
Kampuni
inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika,
lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama
hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu
kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment