Thursday, August 30, 2012

Marais wawili wa chuo leo tulifanya ziara ya kushtikiza katika chuo chetu cha TSJ.

 Bakari Kimwanga Rais (TISJOSO) mwaka 2008-2009. Hapa akiingia chuoni leo akiongozana na Chalila mwandishi wa Tanzania Daima na mwanafunzi wa DSJ mwaka 2006.

Hapa Kimwanga akiwa na Said Mwinshehe, mwandishi nguli wa gazeti Jambo Leo ambae aliongozana na sisi katika ziara hii leo asubuhi.


Kimwanga hapa akitazama ubao wa matangazo huku akifurahia Study Tour ambazo tulikuwa tukiziandaa sana.

 Hapa na mimi niliamua kutokeza katika picha baada ya kukizungukia chuo changu nilichokipenda sana. Nilikaa hapa tangu sijui chocho kuhusu uandishi mwaka 2005, mpaka mwaka 2008, nilipohitimu Diploma yangu.

 Huyu Mzee anaitwa Mwalimu Ramadhan Tonge, ndie alietufundisha upigaji picha. Huu ujuaji wote nilionao katika kupiga picha nzuri huyu ndie alienifundisha kwa miaka mitatu.

 Huyu alie katikati ndie Rais mpya wa chuo (TISJOSO) anaitwa Frida Matinya, ndie Rais wa kwanza mwanamke katika chuo hiki. Hapaamezungukwa na marais waliomtangulia. hakika leo ilikuwa furaha chuoni.

Hapa akijiandaa kunipeleka katika ofisi ya (Times School of Journalism Student Organization) TISJOSO,ambayo mimi ndie nilieifungua kwa mara ya kwanza mwaka 2007, kabla ya hapo TISJOSO haikuwa na ofisi mimi ndie Rais wa kwanza kupigania ofisi mpaka ikapatikana. TSJ ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 eneo la Msimbazi Centre, baadae ikapata majengo ya kupanga eneo la Ilala Sharif Shamba, majengo ya TUICO.

No comments:

Post a Comment