Thursday, August 30, 2012

Hili jembe langu Abdallah James aka Piero aka Kiduchu aka D salut aka jembeeeeee

Huyu ni rafiki yangu wa karibu sana hatujaonana kwa kipindi kirefu yapata miezi sita. Leo amenitembelea nyumbani jioni, tukazungumza mambo mengi sana ambayo nahitaji kuwaeleza hata nyinyi.

Abdallah ametoka Soni kijiji cha wasambaa mkoani Tanga, alikuwa mwalimu lakini katika maisha yake hajawahi hata kusomea japo kozi ya siku moja ya ualimu. Alikuwa anaganga njaa ama kwa maneno yake alikuwa anafukuza upepo.

Ni maisha fulani hivi magumu yasiyo na muelekeo, nilisoma nae kidato cha nne katika shule ya kiislam Masjid Qubah mwaka 1999 mpaka 2002. Sote tukahangaika mpaka tukamaliza shahada mojamoja za chuo kikuu, yeye alisomea shahada ya rasilimali watu mimi nilisomea shahada ya mawasiliano ya umma.

Lakini mpaka sasa hakuwa amepata kazi ya maana, nami kadhalika. Akaniambia sababu ni kuwa sisi hatuna mitandao (connection) ambayo itatuwezesha kujuana na watu ambao watatupa mawazo na fikra mbadala. Abdallah na rafiki yetu mwingine anaitwa Juma Mwiroma walianzisha kampuni ya kupokea tenda za kusambaza vifaa vya kompyuta, lakini waliamua kuifunga kampuni hiyo baada ya kukosa connection kutoka kwa watu.

Hili limekaaje wadau?

Lakini nashukuru leo Abdallah amekuja na habari njema,amenambia amekimbia kule kijijini na amepata kazi Bagamoyo katika hotel, anaweza kuenda kuripoti kazini muda wowote kuanzia leo.....

No comments:

Post a Comment