Saturday, August 25, 2012

Gusagusa mini Band katika mwonekano mpya leo...LEO WAZEE WA KUGUSA GUSA, NIGUSE NAMI NIKUGUSE. NA UKIGUSWA USIONE TABU KUGUSIKA. GUSAGUSA MINI BAND INARUDI TENA BAADA YA MFUNGO WA RAMADHAN KUISHA.

KUMBUKA GUSAGUSA HATUFANYI SHOW ZETU KATIKA MFUNGO WALA KATIKA SIKUKUU.... 

NAAM LEO JUMAMOSI KAMA KAWAIDA TUTAKUWEPO LANGO LA JIJI KUWAPA BURUDANI WAPENZI WETU. TUNAPOSEMA BURUDANI TUNAMAANISHA ILE YA KISTAARAB, MGUU MMOJA JUU, KIJITI MKONONI, TAKSIMA SHAVUNI YAANI FULL HANDAS. 

MCHARUKO WA LEO UTAONGOZWA NA  BBIE MARIAM SHARIF ‘MUHAFAF’ AKIPIGA ULE WIMBO WAKE ADWHIIM 'IWAPI ILE AHADI' (KUMBUKA BIBI MARIAM NDIE MWAFRIKA WA PILI KUFIKIA UWEZO WA UMMU KULTHUM BAADA YA SITTI BINT SAAD, TUMEMTOA ZANZIBAR KWA NDEGE AJE KUIMBA WIMBO HUU TU NA NYINGINE ZITAKAZOPENDEKEZWA NA WAPENZI WETU).

NA MWINGINE NI BIBIE SWABAH SALUM MWINCHACHU, AMBAE NDIE MALKIA WA TWAARAB. MAANA KUNA TAARABU NA TWAARAB. KAMA KAWAIDA ANAJULIKANA BIBI HUYU HAHITAJI MAELEZO.

MWINGINE NI BI AFUAN SULEIMAN AU B52…… SILAHA YA MAANGAMIZI AKISIMAMA LAZIMA UKAE.

HALAFU KUTAKUWA NA SURPRISE MOJA HIYO HATUITAJI. NI MWIMBAJI WA GUSAGUSA ALIEKWENDA UARABUNI KIPINDI CHA RAMADHAN LEO NDIYO ATAREJEA HATUMTAJI NJOO UMUONE.

KITU KINGINE NI BIRTHDAYDAY YA MMOJA WA WAKURUGENZI WA GUSAGUSA. PIA HATUMTAJI NJOO UJIONEE MWENYEWE KEKI ADHWIIIM KUTOKA MOMBASA. CHINI YA UDHAMINI WA ABDUL TRANSPORTER, MWENYEWE ANASEMA KILA MTU AKIINGIA ANA DHARBA MOJA…. YA KIMANI TOKA MOMBASA.

KOSA UCHEKWE...

No comments:

Post a Comment