Saturday, August 18, 2012

Bado vita yangu na ombaomba haijaisha.....

 Huyu ni mwanafunzi wa shule ya msingi akimshangaa huyu mama ombaomba akiwa amejilaza katika kituo cha daladala cha Fire Kariakoo leo mchana.

Hii ni sehemu ya Upanga Kariakoo Fire, wakinamama ombaomba wamejibanza wakisubiri watoto wao waombe ili wawaletee. hapa wanajiburudisha na keki, huyu kijana alievalia nguo nyekundu anawauzia keki.

Kawaida kinamama hawa huwatuma watoto wao wakaombe katika barabara ya morogoro halafu wao wanawasubiri eneo hili. Kinachosikitisha watoto hao ni wadogo sana hawazidi hata umri wa miaka sita.

No comments:

Post a Comment