Afisa mmoja wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba mtandao
wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo umeshambuliwa na wadukuzi (hackers).
Sasa mtandao huo unaonyesha picha na ujumbe kutoka kwa
wanaharakati wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Katika moja wapo ya ujumbe huyo, wadukuzu
wameweka ujumbe kuonyesha kuwa Waziri Mkuu wa Uganda anaomba mashoga radhi kwamba
eti sasa anaunga mkono maandamano ya watu hao wanaofanya mapenzi ya jinsia
moja.
Mapenzi
ya jinsi moja ni hatia nchini Uganda
na wengi ya wanaoshukiwa kuwa miongoni mwao wamekuwa wakishambuliwa na hata
kutelekezwa na jamii.
Mapema
mwaka huu , hoja ya kutaka sheria ibadilishwe na kuongoze adhabu kwa watu
wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kutoka miaka 14 hadi kifungo cha maisha
iliwasilishwa kwa mara nyegine bungeni.
Awali
sheria iliyopendekezwa ilikuwa inasema kwamba yeyote atakaye patikana na hatia
ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na mtoto au mlemavu au mtu anayefanya hivyo
akiwa na ukimwi ,basi adhabu yake ni kunyongwa.
Mtandao
wa kitengo cha sheria na uadilifu nchini Uganda pia unasemekana wiki hii
ulidukuliwa.
Lakini
kamishena wa habari na Teknolojia Bwana Ambrose Ruyooka,aliambia BBC kuwa
tatizo hilo
limerekebishwa.
Serikali
ya Uganda
imenzisha sheria kali ya tovuti na mtandano ilikukabiliana na ufalifu wa
mtandao.
Inandaiwa
kuwa mwanaharakati ajayejiita @DramaSett3r katika Twitter, ndiye anayehusika na
udukuzi huo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment