Saturday, August 18, 2012

Waandishi na wachora katuni wapigwa msasa na wanasheria kuhusiana na kushiriki mabadiliko ya katiba mpya..

Mchora Katuni mahiri Masoud Kipanya na Mmoja wa watangazaji wa kutoka Times FM Radio Ibrahim Issa wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya Wanahabari,Wachora Katuni na Wadau wengine mbalimbali wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani.

No comments:

Post a Comment