Sunday, August 26, 2012

Tanesco bado hawajajielewa.....

Juzi nilikuwa kwa dada Ipty kumsaidia tatizo lake la umeme. Katika nguzo yao nyaya zinaachia hivyo umeme unakatika mpaka aitwe mtu achezeechezee ndiyo unawaka.

Tukaamua kuwaita shirika la umeme Tanzania 'Tanesco' ili waweze kutusaidia katika hilo, lakini cha ajabu walipokuja wakasema hawawezi kupanda juu ya nguzo maana kuna watu wamejenga katika nguzo hiyo. Wakaanza kunifokea ni kwanini tumewaruhusu watu kujenga hapo.

Nikawapa jibu moja tu 'hivi anaepaswa kuwa mkali ni sisi ama nyinyi?' nikaongeza maana kila penye umeme ama nguzo ni eneo lenu, ni mali yenu vipi kila siku mnapita hapa mnaona kuna mtu amejenga na hamumchukulii hatua? Wakanyamaza na kutumia gongo kurekebisha tatizo hilo halafu wakaondoka.

Leo inafika wiki tangu waondoke, lakini sijaona kuwachukulia hatua hawa watu waliojenga katika nguzo zao za umeme.... mhhhhhhh

No comments:

Post a Comment