Friday, August 31, 2012

Mwanamitindo Mustafa Hassanali kukwea pipa... Kuenda Botswana.


Mwanamitindo mkongwe ndani ya Afrika anayetokea Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa katika maonesho ya mitindo ya color in the desert yanayofanyika kuanzia tarehe 31 agost hadi tarehe 1 septemba ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini Botswana katika mji mkuu wa Gaborone. Akiwa ni mtanzania pekee aliyealikwa katika maonesho hayo ya mavazi yanayosifika Botswana  na Afrika kwa ujumla Hassanali anasema “ Nimefurahi sana na anajisikia fahari na heshima kuzindua toleo langu jipya la mtindo ikiwa ni la nne ndani ya mwaka huu na nategemea kutumia fursa hii kuutangaza utamaduni wetu na kuboresha urafiki uliopo kati ya Botswana na Tanzania”.

Toleo hili linaloitwa Pink Desert collection lina magauni yenye alama ya Mustafa Hassanali ikiwa ni pamoja na nguo za kiume ambazo ziko tayari kwa kuvaliwa na kuonesha umaridadi wa mbunifu huyo.


Toleo hili linatoka na kuzinduliwa ikiwa ni kipindi tunachoelekea mwezi oktoba ambao unajulikana duniani kote kuwa ni mwezi wa kuhamasishana dhidi ya ugonjwa wa kansa ya matiti.


‘”Nitatumia toleo hili la mitindo pia katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusiana na tatizo la ugonjwa wa kansa ya matiti ili kila mwanamke aweze kuwa na uelewa wa kujichunguza mwenyewe juu ya afya yake, sambamba na kupenda kuvaa nguo zenye rangi ya pinki kama kiashiria cha uelewa juu ya kansa ya matiti ugonjwa ambao unaathiri wanawake wengi.” Alimalizia Mustafa Hassanali.


Kwa mwaka 2012 Mustafa Hassanali ameshazindua matoleo matatu ya mavazi ambayo ni, Afrikalos aliyoonesha Nchini Nigeria (Lagos), Toleo la Harusi aliloonesha Tanzania (Dar es salaam) na toleo maalumu la mwezi wa Ramadhani liliooneshwa Dakar Senegal.


KUHUSU MUSTAFA HASSANALI 

Licha ya kuwa mbunifu pekee anayeongoza katika ubunifu wa mavazi ya jioni na harusi, Mbunifu nguli wa mavazi Afrika mashariki na kati Mustafa Hassanali anaichukulia fani yake ya ubunifu wa mavazi kama dini hata kufikia kuitwa mkongwe wa ubunifu wa mavazi barani Afrika.

Mustafa Hassanali amekwisha onesha ubunifu wake katika nchi 16 ulimwenguni na miji mikubwa 25 na pia ametajwa katika orodha ya wabunifu bora wa kiume kutoka Afrika ndani ya jarida la new African Woman la nchini uingereza, na pia alichaguliwa na waziri wa habari ,Vijana utamaduni na michezo kuwa katika kamati maalumu ya kutafuta vazi la taifa nchini Tanzania.


Ama kwa hakika Mustafa Hassanali ni mwenye kipaji maalum na asili cha ubunifu wa mavazi.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.mustafahassanali.net
WASILIANA NA: DAVIS MWIJAGE.
SIMU: +255712847881
BARUA PEPE: davis@361tanzania.comi

No comments:

Post a Comment