Friday, August 17, 2012

Leo jembe nilikuwa na waandishi wa mashairi wenzangu katika futari jengo la makumbusho ya Taifa...

 Huyu anaitwa Joe Beda, ni mwanahabari wa gazeti la Tabibu. Alikuwa mhariri wangu wakati nikiandika The African.

 Mwamba huyu Abbas El-Sabry mtangazaji wa Radio Kheir nae alikuwepo katika shughuli hii adhwim.

 Hapanikiwa na jembe langu katika fani ya ushairi anaitwa Mohammed Kinabo ama Mdaiso.


 Watu wakigonga futari haina kuzungumza bali ni vita mwanzo mwisho. Watu wamepiga kuku mpaka wanaona haya.

 Huyu mzee ni mshairi wa siku nyingi,mara baada ya kumaliza futari tu akakamata kalamu na karatasi na kuanza kuandika mashairi ya kuwashukuru wafanyakazi wa Tabibu kwa kutualika futari.



Washairi hapa wakighani vipande vya ushairi kuonysehana ujuzi.

 Huyu mzee baada ya kunogewa na ushairi aliamua kuvua kofia na kuitupa chini ishara ya kukubali fani.

 Huyu ndie mkurugenzi wa gazeti Tabibu akitoa maneno mawili matatu ya kuonyesha shukurani kwa washairi.

 Hapa jembe niliamua kupata picha ya pamoja na wadau huyu alievaa kofia ni Ommar Tego mwanataarab.

 Hapa mkurugenzi wa tabibu aliamua kupata picha ya pamoja na washairi wanawake.

                      Mwamba huwa hajiangushi katika mambo kama haya, hapa akiomba namba ya simu.

Jembe niliamua kuangalia mambo ya makumbhusho, haya ni magari ambayo aliyatumia baba wa Taifa akiwa Rais.

No comments:

Post a Comment