Wednesday, August 29, 2012

leo kama kawaida yangu, nikikudaka tu lazima nikuweke kwenye kidojembe....

 Huyu mzee ni mwanahabari wa siku nyingi sanaaaaaaa... Ni miongoni mwa waandishi walioanzisha ITV, pia alikuwa mwalimu wangu wa habari nikiwa TSJ. Kwa sasa anafanya shughuli za ushauri juu ya habari 'media consultant' Anaitwa Mzee Mbega.

Huyu ni Dada Sabrina Hading'oka, ni mwanahabari Uhuru Radio. Nilisoma nae darasa moja tangu certificate mpaka Diploma katika Uandishi wa habari pale TSJ. Kwa sasa mbali ya utangazi p[ia ni mwanasiasa, juzi aligombea uenyekiti wa NEC UVCCM ngazi ya Wilaya, na amenambia kuwa ameshinda. Hivyo ni mwenyekiti mpya wa UVCCM- NEC Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment