Saturday, August 18, 2012

Leo jembe nimeamkia usafi, maana waswahili husema kanzu ya ijumaa hufuliwa alhamis lakini kanzu ya Eid inafuliwa mwezi 29 ama 30 ya Ramadhan...... Waswahili husema kanzu ya ijumaa hufuliwa alhamis, lakini kanzu ya sikukuu hufuliwa mwezi 29 ama 30 ya Ramadhan. Leo asubuhi nilianza na usafi wa vyombo vilikuwa vimejaa sijaviosha siku tatu. Nikafua nguo na viatu. Baadae nikahamia katika usafi wa nyumba, na pipa la maji lita 2000 nikalisafisha na kumuita mtu wa kujaza maji..... hakika ilikuwa siku ndefu.

 Hapa Jembe nikiwa nimechoka kama kizaa zaa gani. Nimeamka saa 12 asubuhi kufanya usafi, tahamaki imefika saa sita mchana. Ipo haja ya kutafuta mke tuweze kusaidiana kazi jamani khaaa......

Huyu ni baba yangu mdogo anaitwa Abbas El Sabri, mvivu huyooooooo... hajafanya kazi hata moja ila ndiyo amechoka kuliko mtu yeyote nyumbani....

No comments:

Post a Comment