Friday, August 24, 2012

Waislam mpaka sasa hawajui pa kushika kuhusu suala la sensa....

Na Hafidh Kido

 Waislam mpaka sasa hawajakuwa na kauli moja juu ya suala la kupinga sensa baada ya mkanganyiko wa taarifa katika vyombo vya habari kuwafanya waonekana hawana msimamo.

mpaka sasa katibu mkuu wa jumuia ya waislamu Tanzania Sheikh Ponda issa Ponda ameshindwa kukanusha juu ya tangazo lililotolewa katika magazeti mawili ya kila siku juu ya kuwataka waislamu kushiriki sensa.

akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Sheikh Ponda alisema wapo watu wa upande wa pili ambao hakuwataja, kuwa ndiwo wanawaohujumu katika suala hilo.

"Zipo propaganda nyingi juu ya masuala haya, maana yapo matangazo ambayo yanatolewa na watu wasiojulikana kueleza kueleza suala la kukubali kushiriki Sensa na kusema kuwa tangazo hilo limetolewa na katibu wa umuiya lakini hawakutaja jina," alisema.

hata hivyo alipoulizwa juu ya mkanganyoko wa taarifa kwa waislamu alisema wao kama jumuiya msimamo wao upo palepale na hawatetereki kwani serikali haijajenga mazingira rafiki kwa waislamu kuhusu kushiriki sensa.

aidha waandishi walipotaka kujua ni watu wa aina gani ambao wanawahujumu waislamu katika sensa alisema serikali ina njia nyigi za kuwahadaa waislamu kwa kupandikiza taarifa za uongo.

"Msimamo wetu upo palepale na kwani madai yetu ni ya msingi na ili sensa iwe sensa lazima iwahesabu watu wote husika, katika hili tunaona wazi kuwa zoezi la sensa limegubikwa na propaganda na matumizi a mabavu," Ponda.

katika hatua nyingine waandishi walihoji juu ya ujumbe unaosambazwa katika simu unaowataka waislamu kutoshiriki sensa na kubainisha kuwa waislamu wote wafunge siku tatu kuanzia tarehe 23 mpaka 25 mwezi huu na kumalizia na itikafu misikitini.

sheikh Ponda alionekana kutojua juu ya ujumbe huo lakini alieleza kufurahishwa na ujumbe huo kuwa unaeleza habari za kweli kitu kilichoonyesha mpaka sasa waislamu hawana mtu maalum anaehusika na kusambaza taarifa za kupinga sensa.

"Mhh ujumbe huo sijaupata lakini ni mzuri maana unaeleza mambo ya msingi, na hivi ninavyokwambia tupo katika funga, sote tumefunga na hiyo siku ya jumapili tutakaa misikitini kwa dua maalum," Ponda.  

aidha wakati huohuo jumuiya ya amani kwa waislamu Tanzania (Tanzania Peace Foundation) iliyo chini ya mkurugenzi wao Sheikh Sadiki Godigodi imepinga uamuzi wa waislamu kukataa sensa na kuita uamuzi huo ni upuuzi na kukosa mantik.

"Tumefanya uchunguzi na tukagunua ni ujinga kupinga kuhesabiwa, maana katika dini hakuna mahala ambapo inaonyesha kuhesabiwa ni haramu na jambo hii limeanza tangu enzi za uhai wa Mtume SAW," alieleza Sheikh Godigodi katika mkutano mwingine na waandishi wa habari.

vbilevile jumuiya hiya ya Islamic peace foundatin ilingeza kuwa kama waislamu wanaona kuhesabiwa ni kujivua katika dini hiyo basi wanaopinga sensa wanatakiwa kusilimu upya maana tangu uhuru zimeshapita sensa nyingi nao alishiriki bila ya kipengele cha dini kuwemo hivyo nao wamejitoa katika Uislamu nao wanapasa kusilimu upya.

mvutano huu wa kusebabia ama kuthesabiwa kwa waislamu ulianza mara baada ya zoezi la sensa kutajwa mapema mwaka huu na Waislamu wakataka kuwepo na kipengele cha dini katika dodoso ili kuweza kufahamu idadi ya waislamu nchini maana zilikuwepo taarifa zilizotangazwa na kituo cha televisheni ya Taifa TBC kuwa waislamu ni wengi kuliko wakristo hivyo kauli hiyo ikawaudhi waislamu na kutaka kupatikana kwa takwimu za uhakika.

hata hivyo mapema mwezi uliopita mamlaka ya Takwimu Tanzania kupitia mkurugenzi wake Dr Chuwa walitangaza kuwaomba radhi waislamu nchini na kudai kuwa taarifa zilizotolewa na TBC hazikuwa na ukweli wowote kwani tangu uhuru hakuna sens iliyohesabu watu kwa itikadi ya dini kwani kufanya hivyo ni kinyume na katiba inayotamka kuwa serikali haina dini.

zoezi la sensa litaanza usiku wa tarehe 26 mwezi huu litakalodumu kwa siku saba lakini mpaka sasa Serikali haijapata muafaka wa moja kwa moja juu ya ushiriki wa Waislamu katika zoezi hilo hali inayotishia kuvurugika kwa lengo lililowekwa na Serikali.

No comments:

Post a Comment