Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohammed Mpinga, akiwa amepanda pikipiki akiashiria kuzinduliwa kwa mafunzo ya waendesha pikipiki 1000 watakaofunzwa bure kwa udhamini wa kampuni ya Automobile Association Tanzania.
Rais wa AAT Nizar Jivani, akifafanua jambo mbele ya wanahabari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya waendesha pikipiki jijini.
Na
Hafidh Kido
Kamanda
wa polisi kitengo cha usalama barabarani nchini Mohammed Mpinga, amesema kwa
miaka mine tangu pikipiki kuruhusiwa kubeba abiria kumekuwa na ongezeko kubwa
la uingizwaji wa pikipiki kuliko magari.
Mpinga
amesema hayo leo wakati akizindua mradi wa mafunzo ya waendesha pikipiki na
bajaj jijini Dar es Salaam unaofadhiliwa na kampuni ya Automobile Association
of Tanzania ambapo mradi huo utanufaisha waendesha pikipiki 1000 wa jijini
watakaopata mafunzo bure kwa kipindi cha miezi sita.
“Tangu
Serikali iridhie pikipiki hizi kubeba abiria kibiashara mwaka 2009, kumekuwa na
ongezeko kubwa sana
la pikipiki hizi. Katika kipindi cha miaka mitatu yaani 2009-2011 jumla ya
pikipiki 330,882 zilisajiliwa kati ya magari yote 561,190 ikiwa ni asilimia 60.
“Aidha
mwaka 2011 pikipiki ziliongezeka kutoka 43,746 mpaka 85,702 mwaka 2009 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 51 na bajaj nazo ziliongezeka kutoka bajaj 2,124 mpaka
3,259,” alisema.
Akieleza
changamoto wanazokutana nazo kwa ongezeko la pikipiki nchini kamanda Mpinga
alisema ongezeko hili limeongeza idadi ya ajali za pikipiki, wizi na majeruhi
wa pikipiki kwa waendeshaji na abiria.
“Aidha
kwa upande wa ajali kwa kipindi cha miezi mitatu (April, May na June) 2012
jumla ya ajali za pikipiki 1,386 zilitokea na kusababisha vifo vya watu 251 na
majeruhi 1,289,” aliongeza.
Kampuni
ya AAT inayoshughulika na vyombo vya usafiri itagharamia mafunzo ya waendesha pikipiki
1000 katika jiji la Dar es Salaam na kuhakikisha kupunguza tatizo la madereva
wasio na uzoefu ambao mara ningi ndiwo wanaosababisha ajali.
Akizungumzia
mafunzo hayo Rais wa AAT Nizar Jivan anasema ‘tumeamua kupunguza ajali za
pikipiki kwa kufungua mafunzo haya yatakayodumu kwa miezi sita, tutachukua
madereva 30 kila wilaya Temeke, Ilala na Kinondoni. Halafu tutawaachia polisi
kuangalia juu ya utaratibu.
“Kitu
kinachohitajika ni mtu awe na umri usiopungua miaka 18, awe na leseni ya
kuendesha bodaboda, na hata wasio na leseni pia wanaweza kujitokeza. Maana lengo
letu ni kusaidia vijana, mafunzo haya yatakuwa bure bila malipo,” alieleza.
Mafunzo
haya yamekuja wakati muafaka ambapo vifo na ulemavu unaosababishwa na ajali za
pikipiki nchini vimeshamiri, hivyo jeshi la polisi kuonekana kuelemewa na suala
hili maana kila mtu anataka kufanya biashara hii ya pikipiki ili kujipatia
senti.
Hata
kama mtu hana ujuzi wa kuendesha pikipiki atajifunza usiku mmoja na siku ya
pili anapita barabarani na kupishana na magari makubwa hali hana ujuzi wala
elimu ya kukaa barabarani na chombo cha moto.
HAFIDH
KIDO
DAR
ES SALAAM , TANZANIA
0713
593894/ 0752 593894
28/08/2012
No comments:
Post a Comment