Friday, August 31, 2012

Mikoani kuna mambo, hebu soma habari hii...


Kufuatia habari iliyochapishwa katika Gazeti la Majira la tarehe
29-08-2012, na mwandishi, Yusuph Mussa, Korogwe, DC wa Korogwe
aliyetamka maneno hayo
.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Bwana Mrisho Gumbo,
 
anatarajiwa kufikishwa kizimbani wakati wowote kwa madai ya
kumdhalilisha Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi Najum Tekka.

Bi Tekka alifikia uamuzi huo baada ya Bwana Gambo kumwambia Shahada
 
yake ni ya nguo za ndani pamoja na kumuweka chini ya ulinzi wa polisi
ili ahojiwe bila kujua kosa lake.

Akizungumza na gazeti la MAJIRA jana, Bi Tekka alisema kutokana na
 
udhalilishaji huo, anatarajia kufungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda
ya Tanga na kudaia fidia ya Sh 90 milioni.

Alisema Juni 14 mwaka huu Bwana Gambo alimwita kwenye kikao cha kamati
 
ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya, ambacho kilifanyika ofisini kwake
ambapo kikao hicho, pia kilihudhuriwa na baadhi ya Madiwani pamoja na
viongozi wa soko la Manundu Mjini Korogwe.

Sababu ya kuitisha kikao hicho ilikuwa ni kutafuta muafaka kwa njia ya
 
mazungumzo ili kama tutakukubaliana na wafanyabiashara wa soko la hili
ambao wanapinga ongezeko la kodi ya vibanda kutoka 2,000/= kwa mwezi
hadi 20,000/= kwa mwezi ifutwe.

"Majibu yangu katika kikao hiki ndiyo yalimfanya Bwana Gambo
 
kunidhalilisha kwani mimi kama mwanasheria sina uwezo wa kuzungumza
kesi ambayo ipo mahakamani," alisema Bi Tekka.

Alisema baada ya kuzungumza maneno hayo Bwana Gambo alianza kusema,
 
"Huyu Mwanasheria Digrii yake ni ya Chupi, sina imani naye kabisa,
kesi zote za halmashauri anazisababisha yeye, hana msaada wowote
kwetu."

"Kimsingi amenidhalilisha mimi mwenyewe pamoja na taaluma yangu kwa
 
maneno aliyoyatumia, pia amenidhalilisha kwa kuniweka chini ya ulinzi
wa polisi ili nihojiwe wakati kosa langu mimi silijui hata mahakamani
sijapelekwa" alisema Bi. Tekka.

Bi Tekka alisema pamoja na kumpa bwana Gambo siku 14 awe amefuta kauli
 
yake kwa kuitisha kikao kama alichokiitisha awali bado alipuuza, mbali
na kushauriwa na wakuu wenzake wa wilaya.

"Nafungua kesi Kesho (jana) Mahakama Kuu kanda ya Tanga, ili aweze
 
kunilipa Milioni 90 kwa kunidhalilisha" alisema

Bwana Gambo alipofuatwa na MAJIRA alikiri kumualika Bi. Tekka kwenye
 
kikao hicho ili aweze kutoa ufafanuzi kwanini wameshindwa kufikia
muafaka na wafanyabiashara.

"Kabla ya hapo mimi niliwaita wafanyabiashara wakakubali kwenda kufuta
 
kesi, lakini huyu mwanasheria sijui ana maslahi gani na kesi hii,
tulishafikia mwafaka na waende mahakamani kuifuta lakini walipofika
akawakimbia. Hadi sasa kesi haijafutwa lakini wafanyabiashara
wamekubali kulipa sh. 10,000/= badala ya sh.20,000/=, kweli aliandika
notice ya kuomba radhi kwa kumdhalilisha lakini nilimwambia aende
mahakamani hata leo, tutakwenda kupambana " alisema Gambo.

Bwana Gambo alipongeza kuwa, kama Bi.Tekka anadai alidhalilishwa,
 
mbona hakuandika madai hayo polisi badala yake anakaa na watu wake na
kudai amedhalilishwa?

Mwandishi: Prosper R Mushi

No comments:

Post a Comment