Monday, August 27, 2012

Nape aishangaza CHADEMA.....


Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia katibu wake wa itikadi na uenezi Nape Nnauye kimekataa kuomba radhi kwa chama cha upinzani cha Chadema juu ya tuhuma za kudaiwa kutumiwa na nchi za nje kwa kupewa misaada ya fedha ili kuhujumu nchi.

Akizungumza na waandishi wa andishi wa habari leo katika ofisis ndogo ya CCM Dar es Salaam Nape alisema hawezi kuomba radhi na yupo tayari kuenda mahakamani kuthibitisha tuhuma hizo mahakamani.

Nape amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya shilingi bilioni 3 na shilingi moja, za kitanzania kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha nchini.

“Hizo siku saba walizonipa ni ndogo sana mimi nawataka waende mahakami hata leo, lakini wajiandae kumsindikiza katibu mkuu wao ‘Dk.Slaa’ kuenda mahakamani ama kuandaa bilioni 3 na shilingi moja kwa kudai CCM imeingiza kontena la silaha nchini,” alisema Nape.

aliongeza kuwa ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.


Juzi Chadema kupitia mbunge wake machachari jimbo la Ubungo John Mnyika walimtaka Nape Nnauye kukiomba radhi chama hicho au kumtaka kulipa fidia ya Tsh. bilioni 3, kwa madai ya kusema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri.
Ambapo aliendelea kusema kuwa fedha hizo mara nyingi hutolewa ikiambatana na masharti magumu kama kuvuruga amani ya nchi.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/0752 593894
Kidojembe@gmail.com

No comments:

Post a Comment