Ndugu zangu,
Nilipokuwa kidato cha tano
shule ya Sekondari MOA (Mwenge Open Academy ),
nilisoma kitabu kimoja kikitwa ‘Miradi bubu ya wazalendo’ kilichoandikwa na
mwanafasihi maarufu Tanzania
na mshairi wa siku nyingi Ndugu Gabriel Ruhumbika.
Sasa nimekuwa mpenzi mzuri wa
vitabu, natamani kukitafuta kitabu kile lakini sijui nitakipata wapi, ila kama
kawaida yangu nikikipata nitakipiga picha na kukiweka kwenye blogu yenu ili
nanyi kama mtataka kukinunua mukione
kinavyofanana.
Leo nilipotoka ofisini
asubuhi baada ya kikao cha kujadili gazeti letu linalotoka kila jumatano niliamua
kupitia kwa dada ili kupata mazungumzo mawili matatu na kugonga chai, niliamua
kutembea kwa miguu ili niweze kujione Tandale ilivyo, maana nyumbani si mbali
na alipo dada. Kama vituo vitatu hivi, ila
uvivu unatufanya tunaabudu kupanda daladala ama bodaboda, leo nikaamua kuuvunja
mnyororo wa uvivu.
Sikuondoka patupu, kila
nilipopita nilikuta watu wanajituma kuanzisha miradi midogomidogo ambayo
kimsingi huwaingizia chochote. Nikajiuliza swali moja, hivi miradi hii
imesajiliwa ama kurasimishwa na taasisi za kiserikali kama ‘MKURABITA’ (Mpango
wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania )
ili kama watahitaji kusaidiwa ama kuomba mkopo
katika kanzi ‘Bank’ waweze kupata bila matatizo? Ndipo nikakumbuka kile kitabu
cha ‘Miradi bubu ya wazalendo’
Hebu nanyi itupieni jicho miradi
hii na mtoe maoni yenu ikiwezekana…. Kumbuka miradi hii yote ipo sehemu moja
kila baada ya hatua kumi unakutana na mradi mpya unaofanana na wa awali. Je wamepewa
mafunzo ya ushindani wa kibiashara, tatizo lipo wapi kwa wafanyabiashara
wenyewe ama viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na Serikali kuu kupitia
wizara ya viwanda na biashara?
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
22/08/2012
kidojembe@gmail.com
Ndugu Kido,
ReplyDeleteAwali ya yote naomba nikufahamishe furaha yangu kutambua wewe, ulikuwa mpenzi wa kusoma ni wajina wangu. Habari wajina...
Jana majira ya saa tatu na nusu usiku nilihitimisha saari yangu ya kusafiri katika bahari ya simulizi ya Ndugu Ruhumbika katika kitabu chake cha "MIRADI BUBU YA WAZALENDO" nami leo nilikuwa ninashauku ya kutafuta kama mwandishi mwenyewe aliwahi kuandikia kitu kuhusu kitabu hicho hapa mtandaoni na ndipo nilipokutana na huu kurasa wako na makala yako.
Nimefurahishwa sana na kitabu hiki lakini kuna maswali kadhaa wa kadhaa ninayo juu ya mwandishi na hadithi lakini... kwa kuwa nimeona namba yako basi si mbaya naweza kukushirikisha na hata kubadilishana mawazo kidogo.
Jasper "Kido" - Rasmi Jasper, Almaarufu Kido