Saturday, August 25, 2012

Hayaa hayaaaa.... Gusagusa...

 Hapa Bi Afua Suleiman B52 akipagawisha watu na wimbo wake adhwim wa 'pole jirani' au maarufu 'kama ni rahisi ungaliyaanza kuyatenda'

 Naona Eddy Shossy alishindwa kujizuia akaamua aende kutunza maana kweli si rahisi mapenzi kuyaanza na kuyalea. Yataka ufundi na uvumilivu.

 Mkurugenzi wa Gusagusa (katikati) Hassan Farouk akiwa na wageni wake ambayo ilikuwa ni suprise ya jana.

Huyu ni mpiga kinanda na muimbaji wa siku nyingi. Ana historia kubwa katika ucharazaji vinanda. Anaitwa Saleh Amour 'Zungu.' Amefunzwa ufundi huu na Band ya siku nyingi ya All Star, pia aliwahi kuwa na Twanga Pepeta, African Theater TOT na Band nyingi. Alipotea kwa muda kidogo alikuwa nchi za kiarabu akipiga mzigo. Jana alikuwemo katika kuwapa burudani wapenzi wa gusagusa.

Picha Na Abbas El Sabry 'Mwamba'

No comments:

Post a Comment