Kitu nilichojifunza leo ni
kuwa watanzania wengi wanatumia mitandao ya kijamii kujifurahisha tu bila kujua
fursa ambazo zinaweza kuwafanya wakawa matajiri bila ya kuajiriwa.
Mwanaadamu huna budi
kutengeneza bomba ama mrija wa kuzalisha pesa ‘pipe line’ kwani si kila siku
utakuwa na afya ama utakuwa na nguvu za kufanya kazi za sulba. Inahitajika pesa
zako zikutumikie na si wewe kuzitumikia pesa.
Kwa mfano unapogundua
unatumia mitandao ya kijamii bure basi wewe unatumika kama
bidhaa ama njia za wengine kuzalisha pesa kupitia uwepo wako.
Tazama, watu wengi wanaweka
pesa katika kanzi ‘bank’ lakini pesa hizo zinakaa miaka miwili mpaka mitatu
bila ya kuzitumia. Lakini cha ajabu watu wenye shida wanakwenda kukopa na
kuanza kuzitumia. Hivyo huna sababu ya kshindwa kuzizalisha pesa zako.
Umeshawahi kuona kurasa za
kampuni kubwa mfano tigo, vodacom ama Serengeti katika facebook? Basi wapo watu
kazi yao ni
kuziendesha kurasa hizo na wanalipwa mamilioni ya pesa kwa mwezi. Vipi wewe
umesha ‘like’ kurasa ngapi za kampuni, unajua kama
unawaingizia pesa watu kupitia uwepo wako?
Mpaka sasa umeshachukua hatua
gani kuhakikisha furaha yako ya kushiriki mitandao ya jamii haiishii katika
kukutana na marafiki wako ulioachana nao siku nyingi badala yake inakuwa ni
ajira?
Duniani kuna mabilioni ya
blongs na website zinazokaribia 600, wewe upo wapi?
Anza sasa uhakikisha mitandao
ya kijamii kwako ni ajira na si furaha tu.
Tafakari… chukua hatua.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM , TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
kidojembe@gmail.com
Huyu ni mzee Charles Nazi mwandishi wa vitabu juu ya ujasiriamali na pia anamiliki blogu inayohusu namna ya kuwa tajiri.
Semina ikiendelea huku wadau wakisikiliza kwa makini bila kukosa hata kitu kimoja.
Jembe nsmi nikiwa makini wakati wa semina.
Bwana Mlaseko huyu akiendelea kuwapasha watu habari.
Washiriki hawa wakisikiliza kwa makini.
Jembe na laptop yake akiuza sura, kuchoka nako kubaya.
No comments:
Post a Comment