Wednesday, August 29, 2012

Watanzania wangapi tunasoma ama kuandika vitabu? Soma hapa...

 Kutoka kushoto katibu wa mradi wa vitabu vya watoto CBP, Pilli Dumea akiteta na Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya tuzo ya waandishi wa riwaya barani Afrika Shafi Adam Shafi.

 Mwenyekiti wa Chirldren Books Project (CBP) Abdullah Saiwaad akionyesha matangazo ya vitabu vilivyoshiriki mashindano hayo mwaka jana.

 Pilli Dumea akionyesha moja ya vitabu vilivyoshiriki mashindano ya riwaya za kiingereza kwa Tanzania.

 Shafi Adam Shafi mwandishi wa siku nyingi riwaya za Kiswahili, akipitia moja ya vitabu vilivyoshiriki shindano la riwaya za kiingereza. Bwana ameandika vitabu vingi kikiwemo Vuta Nikuvute, Kuli, Barza ya Mwinyi Fuad, Jumba maro na vingi ambavyo sijavisoma bado.

 Huyu ni mwakilishi wa mshindi wa miswada bora minne katika shindano hilo. Alimwakilisha ndugu Israel Yohana aliendaka kitabu 'Tears from lonely heart'

 huyu ni mshindi wa mswada bora wa riwaya zilizoshiriki mashindano, anaitwa Mkama Mwijarubi ambae aliandika kitabu 'Kiss Kiddo: The birthday party'. Kila mmoja alipata dola 2000 za kimarekani. Mshindi mwingine ambae hakufika alikuwa nia Richard Mabala aliendaka mswada ulioitwa 'Run Free'.


 Mkurugenzi mtendaji wa Mkuki na Nyota Publisher Bwana Walter Bigoya akisisitiza jambo katika mkutano huo.

Hapa Shafi Adam Shafi akiwafunda wanahabari juu ya utamaduni wa kujisomea vitabu kwa manufaa ya kila mmoja.CBP Logo
UZINDUZI WA MZUNGUKO WA TANO WA MASHINDANO YA UANDISHI WA RIWAYA ZA KIINGEREZA KWA AJILI YA VIJANA
Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika ni Mradi ulioanzishwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, CODE kwa ufadhili wa Bwana Bill Burts ambaye ni Mkanada.
Madhumuni makubwa ya Mradi huu ni kuwezesha upatikanaji wa vitabu vya kujisomea vitakavyowasaidia wanafunzi walioko katika shule za msingi kujifunza Kiingereza ili kujiandaa kwa elimu ya sekondari ambayo inatolewa kwa Kiingereza.
Aidha vitabu hivyo vinalenga katika kuhamasisha usomaji miongoni kwa vijana, pamoja na kukuza uchapishaji na fasihi ya Kiafrika. Zaidi ya hayo, Mradi unalenga katika kutambua waandishi bora wa Afrika na vitabu bora kutoka Afrika.
Hadi  sasa Mradi umeweza kuchapisha vitabu aina 9 ambavyo ni:
1.      Tree land: The Land of Laughter
2.      The Best is Yet to Come
3.       A Hero’s Magic
4.      Face Under the Sea
5.      Living in the Shade
6.      In the Belly of Dar es Salaam
7.      Close Calls
8.      Lesssilie the City Maasai
9.      The Choice
Miswada bora ya mzunguko wa nne ni:
1.      Run Free - Richard Mabala
2.      Tears From Lonely Heart - Israeli Yohana
3.      Kiss Kiddo: The birthday party - Mkama Mwijarubi.
Hivi sasa miswada hiyo inachapishwa na wachapishaji waliowasilisha miswada hii ambao ni: E& D Vision Publishing, Mkuki na Nyota na Aidan Publishing
Mashindano ya mzunguko wa tano yataanza leo tarehe 29 Agosti, 2012 hadi Machi, 30, 2013, ambapo wachapishaji watatakiwa kuwasilisha miswada yao katika ofisi za Mradi.
Mafaniko ya Tuzo ya Burt ya Fasihi  ya Kiafrika
1.      Tuzo ya Burt imeweza kuchapisha aina tisa (9) za vitabu ambazo ni sawa na nakala 30,000. Vitabu hivi vimesambazwa katika shule 146 zilizoko katika Programu ya Usomaji, maktaba za jamii, na nakala 300 maktaba zilizoko mikoani.
2.      Vitabu hivyo vimeongeza uwepo wa vitabu vya kujisomea shuleni katika lugha ya Kiingereza.
3.      Baadhi ya wachapishaji wameweza kuuza vitabu vyao katika nchi jirani za Afrika Mashariki.
4.      Tuzo hii imewezesha kutambua waandishi mahiri wa lugha ya Kiingereza.
5.      Tuzo hii inaunga mkono Mkukuta kwa kutoa mafunzo kwa wadau na kutoa zawadi nono kwa washindi.
6.      Kwa kupitia Tuzo hii waandishi wa Kitanzania wamehamasika kuandika miswada ambayo inahaririwa  na kuchapishwa kwa ubora wa hali ya juu.
7.      Warsha za waandishi zimewawezesha kujifunza mbinu za uandishi wa riwaya kwa Kiingereza.
8.      Serikali imeweza kuutambua Mradi na kumshukuru mfadhili wa Mradi, jambo linaonyesha heshima kwa mfadhili huyo.
9.        Aina 3 za vitabu chini ya Mradi vimeteuliwa kutumika kama vitabu vya fasihi ya kiingereza kwa madarasa ya kidato cha 3-4 na 5-6 kuanzia Julai 2012. Vitabu hivyo ni Face Under the Sea, The Best is Yet to Come na Tree Land the Land of Laughter.
Changamoto
-          Wachapishaji wengi wa vitabu wako katika miji mikubwa na hasa Dar es Salaam. Mikoani kuna wachapishaji wachache sana. Hali hii inawafanya waandishi chipukizi kutoka mikoani kushindwa kushiriki katika mashindano.
-          Waandishi wengi hawana mafunzo ya kutosha na mbinu mbali mbali za uandishi kuwawezesha kuandika miswada iliyo bora.
-          Tuzo hii inapata ugumu wa kuwafikia waandishi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa nchi.

Wito unatolewa kwa wachapishaji walioko mikoani kutafuta waandishi chipukizi na kuwasaidia ili waweze kushiriki.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/0752 593894
kidojembe2gmail.com/ hafidhkido@yahoo.com
29/08/2012

No comments:

Post a Comment