Marehemu Mpambanaji Daud Mwangosi, katikati akizungumza kitu na mpambanaji mwenzie mitaa ya Iringa enzi za uhai wake.
Hii ndiyo ofisi ya mpambanaji marehemu Daud Mwangosi, tukiifungua ofisi hii maana yake tumemfufua Daud ataishi tena nasi kupitia kazi ya mikono ya mke wake mpendwa pale atakapowasaidia watoto wake.... Lakini kila siku akiwa ananung'unika atakuwa anamkumbuka mume wake, hivyo kila siku atakuwa anakilaumu kifo. Na hiyo haifai... Chukua hatua sasa kumchangia mjane huyu....
Ndugu zangu,
Daud Mwangosi
ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye
tena.
Nimemfahamu Daud
Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa
akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii
kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za
televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au
Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa
shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta
Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku
mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni
mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi
alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali.
Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea
kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio
ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea
kipato kutunza familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko
nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi (
Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina
Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi
angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto
wake pia.
Jana na leo
nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu.
Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi
na wangependa kutoa pole yao
imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi
amefarijika sana
kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari
ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata
photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote
hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo
msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi
milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana na hali aliyo
nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango
hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu
Daud Mwangosi.
Napendekeza
ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa
yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu
tano, ni msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna
rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa,
huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa
Somalia na kuikabidhi UNICEF,
Dar es Salaam .
Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa
kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira.
Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya
kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na
laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo,
usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na
familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama
kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu
kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha
michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754
678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western
Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
No comments:
Post a Comment