Release No. 141
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 6, 2012
Kombaini ya Tanzania ya Copa Coca-Cola imeshika nafasi ya
pili katika kambi ya kimataifa ya michuano hiyo inayoendelea jijini Pretoria , Afrika Kusini. Tanzania
imemaliza mechi za kambi hiyo kwa kufikisha pointi 14.
Ilicheza mechi yake ya
mwisho jana (Septemba 5 mwaka huu) dhidi ya Malawi na kutoka suluhu, matokeo
yaliyoifanya ifikishe pointi 14. Zambia ndiyo iliyokamata nafasi ya
kwanza kwa kufikisha pointi 15.
Mechi hizo zilichezwa
kwa mtindo wa ligi baada ya nchi nyingine kushindwa kwenda Afrika Kusini
kutokana na kuchelewa kupata viza za kuingia za kuwawezesha kuingia nchini
humo.
Mbali ya Tanzania , nchi nyingine zilizowahi kambi hiyo ni
Kenya , Uganda , Nigeria ,
Malawi , Msumbiji ,
Zimbabwe , Zambia na timu
mchanganyiko katika kambi hiyo (CEWA).
Katika mechi zake
Tanzania ilitoka suluhu na Nigeria, ikafungwa 3-2 na Kenya, ikaichapa Zimbabwe
3-0, ikailaza CEWA 3-0, ikaifunga Msumbiji 2-0, ikashinda 2-0 dhidi ya Uganda
na ikafungwa 1-0 na Zambia.
Wachezaji wawili wa Tanzania
wamechaguliwa kwenye kombaini ya kambi hiyo (Dream Team). Wachezaji hao ni
mfungaji bora Basil Seif ambaye ana mabao sita na kipa bora Tumaini Baraka. Pia
Sylvester Marsh wa Tanzania
amechaguliwa kuwa kocha bora katika kambi hiyo.
Makocha watano kutoka
timu ya Chelsea ya Uingereza wanaanza kutoka mafunzo leo (Septemba 6 mwaka huu)
ambapo yatamalizika kesho (Septemba 7 mwaka huu) na timu zitarejea nyumbani
Septemba 8 mwaka huu. k.
Robert Luke Udberg,
Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na Dean Aaron
Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo la makocha.
MKATABA WA UDHAMINI
KUSAINIWA SEPT 11
Mkataba wa udhamini wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itadhaminiwa tena Vodacom utasainiwa Jumanne
(Septemba 11 mwaka huu) kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Taarifa rasmi juu ya muda wa
kusaini na pande zitakazoshuhudia hafla hiyo itatolewa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment