Friday, September 7, 2012

Leo na mimi jembe lenu nilikwenda kuwaaga wanajeshi waliokufa vitani Sudan..

 Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini generali Davis Mwamunyange akitia saini kitabu cha maombolezo Lugalo.



                   Miili ya ndugu zetu ikiwasili katika uwanja wa 34kj leo asubuhi kwa ajili ya kuagwa.


 Ndugu wa marehemu hawa wakisimama kutoa heshima wakati miili ilipowasili uwanjani asubuhi hii.




 Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini akiaga miili ya wapiganaji hao kwa masikitiko makubwa..

 Hapa Mwamunyange akimfariji mmoja wa mtoto wa marehemu hao wakati akimlilia baba yake kwa uchungu mkubwa sana.

Jamani huyu ni shemeji yangu kabisaaaaaaa amemuoa dada Safina Sheshe, anaitwa Kanali Mwami. Mwezi uliopita ndiyo nililala kwake lugalo wakati tulipofiwa na baba yetu Mzee Sheshe ambae amemuoa mama yangu mkubwa. Nae alikuwepo katika kuwaaga wapiganaji wenzie.

 Ndugu na majirani waliohudhuria shughuli hiyo kwa lengo la kuwafariji majirani zao walioondokewa.

 Ndugu wa marehemu wakishindwa kujizuia wakati wakipita mbele ya miili ya ndugu zao....

 Mtoto wa marehemu akipokea nishani ya baba yake iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuheshimu ushujaa wa wanajeshi hao waliofariki vitani Sudan.


                               Generali Mwamunyange hapa akiongea na wanahabari juu ya vifo hivyo.



Na Hafidh Kido

Wanajeshi watatu waliokufa maji Darfur nchini Sudan mwezi uliopita wameagwa rasmi leo katika uwanja wa mazoezi 34 KJ kambi ya Lugalo.

Katika shughuli hiyo ya kuaga iliongozwa na katibu mkuu wa wizara ya ulinzi Job Masima akifuatana na mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Generali Devis Mwamunyange pamoja na mkuu wa jeshi la nchi kavu Meja Generali Salim Mustapha Kijuu.

Wanajeshi hao watatu waliokufa usiku wa tarehe 25 August mwaka huu wakati wakijaribu kuvuka mto Hamada walikuwa ni MT 27919 staff Sajent Julius Chacha Marasi wa kikosi cha (SMI) kambi ya Arusha. Mwingine ni MT 62484 koplo Yusuph Chinguile wa kikosi cha 34 Lugalo, wa tatu alikuwa ni MT 90089 Private Paul Daniel wa kikosi cha 34 Lugalo.

Kwa mujibu wa taarifa za kijeshi wanajeshi hao watatu ni wa battalion ya 6 waliochukuliwa na umoja wa mataifa kuenda kusaidia kulinda amani Darfur ambapo waliondoka tarehe 22 August mwaka huu, ajali iliwakuta wakielekea katika kambi walizopangiwa.

Maana yake ndugu zetu walifariki wakiwa njiani kuenda kuiwakilisha nchi yetu na hawakuwahi hata kuanza kupigana bali walikufa siku ya pili baada ya kuwasili nchini Sudan.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo leo asubuhi Mwamunyange alisema “Hili ni pigo kubwa sana kwa jeshi letu, maana tunachukua muda mrefu sana kuwaandaa na vifo kama hivi vikitokea inatupasa kutafuta watu wengine wenye uwezo kama wao ili kuweza kuwaweka pale walipopungua.”

Nae Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi zilizosomwa kwa niaba yake alisema vifo vya wanajeshi hao inaonyesha ushujaa wa nchi yetu na ujasiri mbele ya mataifa mengine kuwa tupo tayari kufa kwa ajili ya kulinda amani ya bara la Afrika.

Kwa kutambua umuhimu na mchango wa wanajeshi hao katika kulinda amani ya dunia umoja wa mataifa umewatunuku nishani ya ushujaa uliotukuka marehemu hao ambapo wawakilishi katika familia walikuja kuzichukua ikiwa ni kumbukumbu kwao.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
07/09/2012  

No comments:

Post a Comment