Rais wa Marekani
Barack Obama, amewaomba wamarekani kumpa fursa nyingine kuiongoza nchi hiyo.
Ombi lake
amelitoa katika kilele cha kongamano
la chama cha Democratic mjini North
Carolina .
Akijiwasilisha kama mgombea wa urais mwenye
kuleta matumaini kwa wamarekani, Rais Obama alisema kuwa uchaguzi utakaofanyika
mwezi Novemba, utatoa fursa kwa wapiga kura kuchagua kati ya maono mawili
tofauti kuhusu hatma ya Marekani.
Aliwataka
Wamarekani kuwa wavumilivu akisema kuwa matatizo yanayokabili Marekani yamekuwa
yakiongezeka kwa miaka mingi na kuwa itachukua muda kuweza kuyatatua.
Lakini
aliongeza kuwa ikiwa watamchagua tena, ataweza kubuni nafasi mpya za kazi,
kupunguza madeni na kuimarisha uchumi wa Marekani.
Rais
Obama alisema anajiona kama kiongozi aliyekuwa
amewekwa kwa mizani kujaribiwa uongozi wake na kuwa amefaulu. Alisema mpinzani
wake wa Republican, Mitt Romney, hayuko tayari kwa mashauriano ya kidiplomasia.
Alitofautisha
malengo yake na yale ya chama pinzani na kurejelea kauli mbiu yake ya mwaka
2008 , kuwataka watu kuwa na matumaini.
"sikuwahi
kusema kuwa safari hii itakuwa rahisi na sitatoa ahadi hiyo hii leo'' Obama
aliambia kongamano la wajumbe wa Democrat.
Mitt
Romney wa chama cha Republican atapambana na Rais Obama kuwania urais huku kura
za maoni zikionyesha wawili hao wakikaribiana.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment