Tuesday, September 4, 2012

Mzee Wakulyamba huyu jamani....


Ndugu zangu
Jamani usimdharau mtu hata kidogo. Huyu bwana nilikuwa nae Kampala tukisoma pamoja. Yeye alikuwa akifanya Sheria nami kama kawaida uanahabari. Sasa nilikuwa nikimchukulia mtu wa kawaida tu, nae alijaa masikhara wala hakujikweza.

Nilishiriki nae vikao vingi vya siri katika kukijenga KIUTASA chama cha watanzania chuoni, na alionekana ana mawazo ya kimapinduzi kweli. Alimaliza mbele yangu mwaka jana.

Leo nilipokuwa makao makuu ya jeshi la Polisi nikichukua habari nikamuona amekaa, kama kawaida nikamfata na kumsalimia kwa hesima zote. Yeye akarudisha yale masikhara yake ya zamani. Lakini niliogopa maana alikuwa amezungukwa na mavyeo mwili mzima na askari pale makao makuu walikuwa wamemkaukia ajabu.

Nilibadilishana nae namba za simu na kuahidi kuja kumtembelea siku nyingine. Lakini nimejifunza kitu, unapokaa na mtu mahala usimdharau.


No comments:

Post a Comment