Tuesday, September 4, 2012

TIGO KUDHAMINI SARAKASI ZA MAMA AFRIKAkutoka kushoto Afisa habari wa Tigo Alice Maro, Mtaalam wa Mahusiano na Udhamini wa Tigo Edward Shila na Mkurugenzi wa Mancom Costantine Magavilla, wakitoa taarifa hiyo leo asubuhi jijini Dar es salaam.


 Na Jonas Minja
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imedhamini maonyesho ya sarakasi ya mama Afrika ambayo yanatarajia kuanza kufanyika Semptemba 27 mwaka huu katika kituo cha Mancom kilichopo katika viwanja vya ukumbi wa New Cinema Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mtaalam wa Mahusiano na Udhamini wa Tigo Edward Shila, amesema kwamba wanafuraha kupata nafasi hiyo ya kuwa wadhamini wakuu wa sarakasi za mama afrika 2012, tukio ambalo litaamsha hisia za watu kutoka sehemu mbalimbali za tanzania na kuweka kumbukumbu ya burudani kwa kipindi cha mwezi mzima na wanaamini sarakasi za Tigo Mama Afrika ni moja kati ya maonyesho yenye ubunifu na ubora zaidi na wanajivunia kuwa sehemu ya  maonyesho hayo.

Aidha ameendelea kusema kwamba Sarakasi hizo zitaambatana na programu ya nyimbo za kitamaduni na za kisiasa, upindaji wa viungo, michezo ya viinimacho, michezo ya angani na itasindikizwa na muziki wa moja kwa moja kutoka kwa bendi ya In Afrika.

Naye Mkurugenzi wa Mancom Costantine Magavilla, amesema hili ni tukio la kusheherekea na wanaishukuru  kampuni ya Tigo kwa kudhamini  na wana uhakika mchango wao hautoleta tu gumzo kwa watu bali pia kuzikusanya familia za watanzania katika burudani iliyobobea.

No comments:

Post a Comment